Vicheko vya Matumaini?

Ni matumaini yetu kwamba waheshimiwa kwenye picha hapo hawacheki kwa unafiki, bali ni kwa mapenzi ya nchi yao ya Kenya. Wahenga walisema “Asiyekubali kushindwa si mshindani”, hivyo basi, tunafarijika kuona Kambi ya upinzani ya chama cha CORD kinachoongozwa na Mh. Raila Odinga kimekubali kushindwa na kimetaka Wakenya wasonge mbele kwa mustakabali mzima wa maendeleo ya Kenya.

Pichani, ni Mh. Uhuru Kenyatta, Rais mpya wa Kenya, Mh. William Ruto, Makamu wa Rais, Mh.Raila Odinga, waziri mkuu aliyemaliza muda wake na Mh. Kalonzo Musyoka, Makamu wa Rais aliyemaliza muda wake.

Thehabari.com inawatakia Wakenya Kila la kheri katika kujenga na kuendeleza nchi yao.

20130414-120856.jpg