Kesi ya mwandishi ‘kuomba rushwa’ yaairishwa

Na Mwandishi Wetu

KESI inayomkabili mwandishi wa habari ambaye ni mtangazaji wa Shirika la Utangazaji nchini

(TBC1),Jerry Muro na wenzake imeshindwa kuendelea leo kutokana na kutokuwepo kwa wakili wa

upande wa mashtaka.

Kesi hiyo imetajwa leo Machi 7, 2011 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa ajili ya

mashahidi wa upande wa mashtaka kuendelea kutoa ushahidi wao ambapo ilipangwa kusikilizwa

kwa siku mbili.

Akihairisha kesi hiyo leo mahakamani hapo Hakimu Mkazi, Gabriel Mirunde, alisema wakili wa

upande wa mashtaka, Stanslaus Bonniface hayupo kwani yupo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es

Salaam, hivyo kesi inahairishwa.

Kes hiyo imepangwa kuendelea kusikilizwa Machi 8, 2011, ambapo mashahidi wa upande wa

mashtaka wataendelea kutoa ushahidi wao. Washtakiwa katika kesi hiyo Muro na wenzake

wanatuhumiwa kuomba rushwa ya sh. milioni 10 Michael Wage ili asirushwe kwenye kipindi

kutokana na maovu anayoyafanya kazini.

Washtakiwa katika kesi hiyo mbali na Muro, wengine ni Deogratius Mgasa na Edmund Kapama,

ambapo kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani Februari 15, mwaka jana wakikabiliwa na

mashtaka matatu ya kula njama za kutaka kupokea rushwa na kujitambulisha visivyo.

Wage enzi hizo alikuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.