Na Janeth Mushi, Arusha
KESI ya kupinga matokeo ya ubunge wa Godbless Lema (CHADEMA) Jimbo la
Arusha Mjini, imekwama kuanza usikilizwaji wa awali tena hadi
Jumatatu ijayo baada ya mahakama hiyo kushindwa kuwasilisha nyaraka
muhimu, zilizokuwa zinahitajika kwa mawakili wa upande wa wadaiwa.
Kesi hiyo inayosikilizwa katika mahakama kuu Kanda ya Arusha, Jaji
anayesikiliza kesi hiyo Aloyce Mjulizi, akiahirihsa kesi hiyo jana
mahakamani hapo alisema Wakili wa upande wa walalamikiwa Method
Kimomogolo, aliomba kupewa nakala ya uamuzi mdogo ambayo Jaji huyo
uliotupilia mbali pingamizi za awali lililowekwa katika kesi hiyo.
Aidha Kimomogolo aliomba kupewa nakala ya mwenendo wa kesi hiyo
lakini hadi kesi hiyo ilipotajwa jana asubuhi upande wa walalamikiwa
haukuwa umepata nakala hizo.
Kimomogolo aliieleza mahakama hiyo kuwa hawajapewa nakaal hiyo ya
uamuzi mdogo uliotolewa na Jaji kwani wameelezwa upande wa mahakama (wachapaji) wameshindwa kuzichapa nakala hizo kutokana na kubanwa na kikao cha Mahakama ya Rufaa ambacho bado kinaendelea mjini hapa.
Alidai kuwa jana wangeweza kupatiwa nakala hiyo ya uamuzi mdogo wa
pingamizi alizotoa Jaji huyo huku mwenendo mzima wa shauri hilo
wakielezwa kuwa wanaweza kupatiwa ndani ya wiki hii.
Upande huo wa wadaiwa uliiomba maakama hiyokuahirisha kesi hiyo hadi
watakapopatiwa nakala hizo ili wazipitie kwa hatua ya usikilizwaji wa
awali kwa mujibu wa sheria. Katika uamuzi wake wa kuahirisha kesi hiyo, Jaji Mjulizi alimwagiza msajili wa mahakama kutoa nakala hizo kwa wadaiwa na wadai kabla ya kuanza kusilikiza kesi hiyo wiki ijayo.
Alimwagiza pia msajili wa wilaya kutoa taarifa ya shauri hilo kwa
mujibu wa sheria na kubandika kwenye ubao wa matangazo mahakamani hapo na kuomba ukumbi mkubwa wa kusikilizia kesi hiyo kutokana na idadi kubwa ya watu wanaofika mahakamani kusikiliza shauri hilo.
Jaji huyo alimwagiza Msajili huyo pia kuweka utaratibu wa mwenendo wa
shauri hilo kusikilizwa kwa vipaza sauti ili watu waliopo nje ya
chumba cha mahakama walioshindwa kuingia ndani kutokana na ufinyu wa
nafasi waweze kusikia kinachoendela mahakamanai.
Mujulizi alitoa maagizo hayo baada ya wakili wa upande wa wadai
unaoongozwa na Alute Mughwai, kuikumbushia mahakama kuhusu muda
uliopangwa kusikiliza kesi hiyo hadi Disemba kuwa ni mdogo.
Kutokana na hali hiyo aliomba mahakama hiyo iandae utaratibu wa kuomba muda wa nyongeza, kutoa taarifa ya siku ya kesi kwenye ubao wa
matangazo, na kesi hiyo isikilizwe kwenye ukumbi mkubwa zaidi.
Awali Wakili Mughwai alilalamikia suala la usalama mahakamani hapo
lakini wakati akitoa ombi hilo, sauti za kumsonya zilisikika kutoka
kwa watu waliokuwa wamekaa nyuma yake, ambapo alimweleza Jaji huyo kuwa hali hiyo inaonyesha kuwa watu hao wanataka asizunguze jambo ambalo alidai kuwa siyo utaratibu wa kuendesha kesi mahakamani.
Mujulizi alimweleza Mughwai kuwa, “hawakusonyi wewe ila wanaisonya
mahakama,” na baada ya kusema hivyo watu hao walisikika wakipiga
makofi, lakini baadaye Jaji alionya kwamba anayefanya kitendo hicho
ameidharau mahakama. Sahuri hilo limeahirishwa hadi Octoba 24 mwaka huu ambapo linatarajwia kuanza usikilizwaji wa awali.