Kero ya Maonesho ya Biashara ya 37 ya Sabasaba 2013

Eneo maalumu la maegesho ya vyombo vya usafiri kama magari, pikipiki na baiskeli kwa watu wanaofika kutembelea maonesho ya 37 ya biashara ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

HII huenda ikiwa ni miongoni mwa kero ya Maonesho ya 37 ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Wameweka utaratibu mzuri wa uegeshaji magari ya wateja katika viwanja hivyo, lakini bei ya uegeshaji magari na hata pikipiki na baiskeli ni moja tu eti shilingi 4,000.
Hili ndilo tatizo kubwa haiwezekani mamlaka ya biashara ikawa kipofu haijui tofauti iliyopo kati ya vyombo hivi yaani gari, pikipiki na baskeli. Inaonesha utaratibu umewekwa kwa maslahi ya kibiashara zaidi bila kujali tukio linalofanyika katika eneo hilo. Baskeli haiwezi kuwa sawa na gari au pikipiki na hata gari. Kuna kila sababu kwa vyombo hivyo vya usafiri kila kimoja kuwa na bei yake.
Viongozi waandaaji wa maonesho haya wajipange na kuacha kutoa mianya ya watu kutumia fursa hiyo kuwakamua watanzania hasa wa kipato cha chini.Huu ni mtazamo tu…!