*Timu nne zaingia kwenye kipindi cha tatu wiki ijayo
MACHI 28, 2013, Dar es Salaam; Jana usiku kupitia Televisheni za ITV na Clouds TV mashindano ya GUINNESSĀ® FOOTBALL CHALLENGEā¢ yalituonesha ni kwanini ushirikiano ni muhimu kwa washiriki kuonyesha ujuzi wao. Francis Ngigi and Kepha Kimani kutoka Kenya walifanikiwa kuingia hatua ya mwisho na kujipatia fedha za kimarekani dola 3,000 shukrani kwa vipaji vyao na ushirikiano mzuri.
Francis na Kepha wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita cha fedha za kimarekani hadi kufikia dola 250,000. Katika kipindi kijacho cha mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi na kutambulika kama wachezaji na si tu mashabiki, watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Pan-African.
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV. Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku ambapo Clouds TV itarusha kipindi hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku.
Tafadhali kunywa kistaarabu – Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.