NDEGE za kivita za Jeshi la Kenya zimeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Al-shabaab katika taifa jirani la Somalia, taarifa kutoka jeshi hilo zimesema.
Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya Jimbo la Gedo,linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza. Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao kupanga mshambulizi nchini Kenya.
Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini hadi sasa hawajafanya hivyo. Hili ni shambulio la kwanza la Kenya kwa shambulizi la Al-shabaab ambalo lilisababisha mauaji ya watu 148 katika Chuo Kikuu cha Garissa wiki iliopita.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi. Msemaji wa Jeshi la Kenya, David Obonyo ameviambia vyombo vya habari kwamba Jeshi la Kenya lilijibu vitisho kwa kutekeleza mashambulizi ya angani siku ya Jumapili usiku katika eneo hilo. Hakuna maelezo zaidi ya oparesheni hiyo yaliotolewa.
-BBC