Kenya yaionya Al-Shabaab kupitia Tweeter

Wanajeshi wa Kenya wakiwa kazini

MSEMAJI wa Jeshi la Kenya kwa kutumia Twitter ameonya wakazi wa miji 10 nchini Somalia kuwa “watashambuliwa vikali, mfululizo”.

Msemaji huyo Meja Jenerali Emmanuel Chirchir, ameiambia BBC kuwa miji hiyo – ni pamoja na Kismayo na Baidoa – ambayo ni ngome ya kundi la al-Shabaab.

Taarifa kutoka Kenya zinasema Kenya imetuma wanajeshi nchini Somalia mapema mwaka huu, kwa sababu inalaumu kundi la al-Shabaab kwa wimbi la utekaji nyara. Al-Shabaab, ambayo inadhibiti eneo kubwa la upande wa kusini, inakanusha madai hayo.

“Jeshi la Kenya linatoa wito kwa yeyote anayeishi au mwenye jamaa na marafiki wa miji 10 kuwashauri,” Meja Emmanuel Chirchir aliandikwa kwenye ukurasa wake wa Twitter. Hata hivyo miji aliyoitaja ni tisa ambayo ni Baidoa, Bardhere, Dinsor, Afgoye, Buale, Barawe, Jilib, Kismayo na Afmadow.
-BBC