
Wapiganaji wa kundi la Al Shabab
MAKAMO wa Rais wa Kenya, William Ruto, amesema kuwa askari wa usalama wa Kenya wamewaandama wapiganaji wa Al-Shabaab hadi kwenye kambi yao nchini Somalia, baada ya shambulio dhidi ya basi Kaskazini – Mashariki mwa Kenya hapo jana ambapo raia 28 wa Kenya waliuliwa.
Ruto alisema wapiganaji zaidi ya 100 wa kundi la Al-Shabaab waliuliwa katika operesheni mbili tofauti zilizofanywa na askari wa Kenya. Alisema kambi ya Al-Shabaab iliangamizwa katika operesheni hiyo.
Hata hivyo habari hizi hazikuthibitishwa na upande wa Al-Shabaab. Gavana wa Mandera – ambako shambulio la jana lilitokea – amelaumu vikosi vya usalama kwa Kenya kwa kushindwa kuwalinda raia wake. Alisema polisi kawaida wanashindwa kufanya uchunguzi kamili baada ya mashambulio hilo.
-BBC