
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Dk. Edmund Mndolwa (kushoto) akimkabidhi moja ya kitanda cha kujifungulia wajawazito, Daktari Mfawidhi wa hospitali ya Buguruni, Hawa Lesso wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya hospitali hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine katikati ni Mkurugenzi wa KCB, Moezz Mir na Mwenyekiti wa Hospitali hiyo Fatma Faki.

Mkurugenzi wa Mtendaji KCB Tanzania, Moezz Mir akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 13 Mkurugenzi Msaidizi wa Hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla kwa ajili ya kununulia vifaa mbalimbali vya hospitali wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Dk. Edmund Mndolwa.