Kaymu yafungua Tawi Jipya la Huduma Kariakoo

Meneja wa Kaymu nchini Tanzania, Erfaan Mojgani akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo kipya cha huduma cha Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Utendaji na Uratibu wa Kaymu Tanzania, Bi. Ulumbi Bryceson.

Ofisa Utendaji na Uratibu wa Kaymu Tanzania, Bi. Ulumbi Bryceson akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo kipya cha huduma cha Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Kaymu nchini Tanzania, Erfaan Mojgani.

Mmoja wa wauzaji wanaotumia mtandao wa Kaymu, Zacharia Massawe (kulia) kutoka duka la Classic Shoe, Kariakoo akielezea alivyonufaika na uuzaji kwa kutumia mtandao wa Kaymu. Kushoto ni Meneja wa Kaymu nchini Tanzania, Erfaan Mojgani.

Mmoja wa wauzaji wanaotumia mtandao wa Kaymu, Zacharia Massawe (kulia) kutoka duka la Classic Shoe, Kariakoo akielezea alivyonufaika na uuzaji kwa kutumia mtandao wa Kaymu. Kushoto ni Meneja wa Kaymu nchini Tanzania, Erfaan Mojgani.

Meneja wa Kaymu nchini Tanzania, Erfaan Mojgani akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo kipya cha huduma cha Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Utendaji na Uratibu wa Kaymu Tanzania, Bi. Ulumbi Bryceson.

Meneja wa Kaymu nchini Tanzania, Erfaan Mojgani akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo kipya cha huduma cha Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Utendaji na Uratibu wa Kaymu Tanzania, Bi. Ulumbi Bryceson.

Baadhi ya wafanyakazi wa tawi jipya la huduma kwa wateja wa kampuni ya Kaymu wakiwa katika majukumu. Kaymu inafanya kazi ya kuratibu usafirishaji wa bidhaa za wanunuaji na wauzaji zinasafirishwa kwa muda unaotakikana.

IMG_0023

Na Mwandishi Wetu

KAYMU Tanzania imefungua tawi jipya Kariakoo ambalo litafanya kazi kama kituo cha kuweka bidhaa kabla hazijasafirishwa kwenda katika maeneo husika.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Tawi hilo jipya, Meneja wa Kaymu nchini Tanzania, Erfaan Mojgani alisema kufunguliwa kwa tawi hilo kupunguza usumbufu ambao awali wauzaji walikumbana nao katika kupata huduma stahiki za kampuni hiyo. Akifafanua zaidi Mojgani alisema tawi hili jipya liko sambamba na mkakati wa kampuni wa kuleta huduma karibu na wauzaji nchini pote.

Aidha alisema ofisi hiyo mpya ya tawi ambayo iko Kariakoo mtaa wa Congo. “Hii ni ishara kubwa wa ukuaji wa biashara hapa Tanzania na ni uwekezaji wa ziada nchini kuhakikisha mafanikio kwa wanunuzi na wanunuaji,” alisema Mojgani.

“…Tunajivunia kuwa karibu zaidi na wateja wetu; hii itasaidia sana katika mchakato wa usafirishaji bidhaa kwa kuwa tupo karibu zaidi na maduka ya wauzaji wengi. Ofisi hii inatazamiwa kutumika katika huduma za usafirishaji kila siku za kazi na pia katika kutoa huduma nyingine kama kujibu maswali ya wateja, kutoa mafunzo kwa wauzaji na kuwa na vifaa vya kutolea huduma za upigaji picha zenye ubora zaidi,” aliongeza meneja huyo.

Naye mmoja wa wauzaji wanaotumia mtandao wa Kaymu, Zacharia Massawe kutoka duka la Classic Shoe, Kariakoo alisema wamefurahishwa na kitendo cha Kaymu kufungua kituo chake cha huduma Kariakoo kwani huduma watazipata jirani na kwa haraka.

“Tumefurahishwa sana na hatua ya Kaymu kufungua kituo chake hapa Kariakoo. Huu mchakato mpya utatusaidia sana katika kutimiza oda zetu kwa wingi. Naamini itatusaidia katika kukuza biashara zetu,” alisema Massawe.

Kwa upande wake Ofisa Utendaji na Uratibu wa Kaymu Tanzania, Bi. Ulumbi Bryceson akizungumza na waandishi wa habari alisema kufunguliwa kwa tawi hilo jipya kutasaidia usafirishaji wa bidhaa za wateja kwa pamoja hivyo kuondoa ucheleweshaji wa bidhaa kwa wateja.

“Hii ni njia nyingine ya kuwasaidia wadau wenzetu wa usafirishaji bidhaa, kwa kuwa inawawezesha kuchukua bidhaa nyingi kwa wakati moja kutoka eneo moja maalum, na hivyo kupunguza ucheleweshwaji katika usafirishaji bidhaa ama kughairi kushughulikia oda kutokana na maeneo ya wauzaji husika kutokujulikana,”

Kaymu inafanya kazi na wadau mbalimbali kuhakikisha bidhaa za wanunuaji na wauzaji zinasafirishwa kwa muda unaotakikana. Uanzishwaji wa ofisi mpya unachangia huduma za uhakika za usafirishaji.