KATIBU WA BUNGE ZIARANI GHANA


Katibu wa Bunge la Tanzania akiwa Mwenyekiti wa kikao cha Tathimini ya Maandalizi ya Mkutano wa kwanza wa Makatibu wa Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola utakaofanyika nchini Ghana. Upande wa kushoto ni wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano toka Bunge la Ghana, upande wa kulia ni Maofisa wa Sekretarieti ya chama hicho barani Afrika. Kikao hichi kilifanyika katika Bunge la Ghana mjini Accra.

Katibu wa Bunge la Tanzania ambae pia ni Katibu wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola barani Afrika, Dr.Thomas Kashililah (mwenye miwani) akimkabidhi Katibu wa Bunge la Ghana, Emmanuel Anyimadu vitabu vya Mpango Mkakati (Strategic Plan) wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA).

Katibu wa Bunge la Tanzania, Dr. Thomas Kashililah(wa pili kulia) akiwa na Katibu wa Ghana, Emmanuel Anyimadu wakiwa na siwa ambayo ni ishara ya mamlaka kamili ya Bunge la nchi hiyo. Katibu wa Bunge la Tanzania yuko Ghana kwa nafasi yake kama Katibu wa Bara la Afrika wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola akiwa ameenda huko kutathmini maandalizi ya Mkutano wa kwanza wa Makatibu wa Mabunge wanachama wa Chama hicho kanda ya Afrika. Wengine pichani kutoka kushoto ni Saidi Yakubu (Mratibu wa chama hicho barani Afrika), Demetrius Mgalami (wa pili kulia) ambaye ni Naibu Katibu wa Bara la Afrika wa Chama hicho, na wa kwanza kulia ni Robert Okudo, Naibu Katibu wa Bunge la Ghana.