KATIBU MKUU WIZARA YA VIWANDA , BIASHARA NA MASOKO BI. JOICE MAPUNJO KATIKA UZINDUZI WA MUONEKANO MPYA YA BIA YA SERENGETI, 28TH JANUARI 2012,

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Richard Wells na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Tanzania, Joyce Mapunjo

TUATAMBUA fika mchango mkubwa wa Kampuni ya Bia ya Serengeti katika kukuza na kuendeleza uchumi wa taifa letu. Serengeti ni moja kati ya kampuni zilizojenga historia kubwa ya mafanikio katika sekta binafsi, nimefurahishwa kuwa pamoja nanyi leo.
Hakika leo sote tunakiri na kushuhudia mafanikio makubwa katika kampuni hii ingawa kuna makampuni mengi makubwa ambayo yanatengeza bidhaa na kuleta ushindani katika soko la kimataifa, hata hivyo haishii kwenye ubora tu bali ufungwaji,upakiaji na uwasilishaji. kwa njia rahisi ili kulifikia soko.
Bidhaa kama hii tuliyoshuhudia uzinduzi wake leo, sisi ni mashahidi kuwa bidhaa hii ni nzuri na hakika itavuka mipaka na kufikia masoko yaliyo nje ya mikapaka yetu, siku zote nimekua nikiitaja kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuleta mabadiliko kwa bidhaa bora ambayo inaleta changamoto ya biashara na furaha ya kipekee kwa wateja wake.
Nakubali kuwa uwekezaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti imeleta ongezeko kubwa katika uchumi wa taifa na mafanikio katika jamii ya watanzania. Kwa uhakika zaidi naliweka wazi kuwa mbali na Kampuni ya Bia ya Serengeti kuajiria Watanzania 1,000, pia kampuni hii inajihusisha moja kwa moja na shughuli za kijamii na kuhamasisha mabadiliko ya kiuchumi kwa kila Mtanzania.
Nimehabarishwa kwa ufupi kuhusiana na Ufunguzi wa kiwanda cha Moshi kuwa kimetengeza ajira 1000 kwa wafanyakazi wa kudumu na wale wa muda mfupi ambapo imeongeza wigo wa maendeleo nje ya Dar es Saalam kwa kuzingatia Serikali. Kwa Hatua hii nachukua nafasi kuipongeza bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya bia ya serengeti kwa ufunguzi wa kiwanda cha moshi mwishoni wa mwaka uliopita, ambacho kilifunguliwa na mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengi Pinda. Napenda kuwahakikishia kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu wa maendeleo na sekta binafsi kitaifa na kimataifa.
Napenda kuitambua DIAGEO/EABIL Kwa thamani na mchango mkubwa inayotoa kwa ongezeko la kibiashara na uwekezaji katika mkoa wetu na jamii ya Africa Mashariki. Jukwaa hili linaongeza ushirikiano na kuinua uchumi na maendeleo ya biashara katika hapa nchini. Nipo mstari wa mbele kutoa ushirikiano utakaowezesha bidhaa yetu kusimama katika soko la ndani na nje ya mipaka yetu.
Mabibi na Mabwana, namalizia kwa kusisitiza kwa mara nyingine kupitia tukio hili kubwa la heshima linalotokea nchini kwetu wakati huu kuwaomba wawekezaji waige mfano wa huu ili kwapamoja tuweze kushirikiana katika kuinusuru taifa letu kuanguka au kushuka kiuchumi.
Asante sana kwa kunisikiliza