Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ndani ya Maonesho ya 36 ya Biashara

Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (kushoto) akimwonyesha Katibu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kulia) machapisho mbalimbali jana jijini Dar es salaam ambayo yatumika katika kuwaelimisha wananchi wanaotembelea banda hilo wakati wa maonyesho ya 36 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijja akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Benki ya Posta Fatma Majid juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo kwenye maonyesho ya 36 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam wakati Kiongozi huyo alipotembea Taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Wizara ya Fedha jana jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijja(katikati) akikata utepe jijini Dar es Salaam kuzindua maadhimisho ya miaka 40 tangu Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kilipoanzishwa. Maadhimisho hayo yamefanyika katika banda la Wizara ya Fedha kwenya maonyesho ya 36 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam. Wengine ni Rais wa Wanafunzi IFM Michael Charles (kushoto) na Mkuu wa Chuo cha IFM Profesa Godwin Mjema (wa pili kutoka kulia)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijja akifungua pazia jana jijini Dar es Salaam kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya miaka 40 tangu Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kilipoanzishwa. Maadhimisho hayo yamefanyika katika banda la Wizara ya Fedha kwenya maonyesho ya 36 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam