Katibu Mkuu EAC Afungua Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya Habari Arusha

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), Balozi Dk. Richard Sezibera akizungumza katika mkutano wa Siku mbili kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.


Washiriki wa kongamano la  siku mbili la Uhuru wa Habari Duniani wakijiandikisha kabla ya kuanza rasmi kwa mkutano wa Siku mbili katika kuadhimisha Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani linalofanyika jijini Arusha katika Hoteli ya Naura Springs.

Mgeni rasmi katika siku ya Uhuru wa Habari Duniani Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki  Dr. Richard Sezibera akiwasili na kusalimiana na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha  kufungua Kongomano la siku mbili la Uhuru wa vyombo vya habari kwa wahariri na waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa habari

Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen akisalimiana na  Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki  Balozi Dr. Richard Sezibera mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha kufungua Kongamano la siku mbili la wahariri na wanahabari pamoja na wadau wa habari katika kuadhimisha  siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ulimwenguni.

MC katika Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya habari ulimwenguni Usia Nkoma kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akitambulisha meza kuu ya wageni katika kongamano hilo.

Meza Kuu ikiongozwa na Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera (wa pili kulia) na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen (wa tatu kushoto).

Picha juu na chini Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi  Dr. Richard Sezibera akihutubia na kufungua Kongamano la Siku Mbili linaloenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani.

Na Mahmoud Ahmad Arusha

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), Dk. Richard Sezibera leo amefungua rasmi kongamano la waandishi wa Habari Tanzania pamoja nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika kuadhimisha ya siku ya uhuru wa vyombo vya Habari Duniani uliobeba kauli mbiu “USALAMA NA MAZINGIRA BORA YA KUFANYIA KAZI KWA WAANDISHI WA HABARI NA WAARIRI AFRIKA YA MASHARIKI”

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kaongamano hilo la waandishi wa habari liliofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Naura springs amesema kuwa kongamano hili la vyombo vya Habari pamoja na wamiliki lina umuhimu kwa sababu litaifanya jamii pamoja na serikali kujua nini umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika maendeleo ya nchi na jamii yote.

Amesema kuwa uhuru wa  vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa unajikita katika uhuru wa kutoa maoni na pamoja na uhuru wa  kutoa habari  hivyo katika kuelewa hilo vyombo vya habari vinatakiwa viwe vinafanya kazi zake pasipo kutegemea upande wowote ili kisije kuchochea au kuvunja amani ya nchi kama ilivyotokea miaka ya nyuma kwa nchini Rwanda na Burundi.

Aidha amesema kuwa kuna changamoto kubwa sana zinazozikumba vyombo vya habari hususani vyombo vya kijamii  ambapo wanakuwa na mazingira magumu ya kutafuta habari na kufanya wakati mwingine waandishi kuwa katika mazingira hatarishi kwa maisha yao pamoja na hali mbaya ya kiuchumi inayopelekea kutoweza kufanya kazi kuendana na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia ikiwepo kujiingiza katika mawasiliano ya mkongo wa kitaifa.

Kongamano la mwaka huu limeratibiwa na  MISSA TANZANIA kwa kushirikiana na  EAJA, Mfuko wa vyombo vya Habari Tanzania ( TMF), Muungano wa club za wandishi wa habari (TPC), Umoja wa Mataifa Tawi la Tanzania, Baraza la Habari Tanzania (MCA), Wamiliki wa Vyombo vya habari Nchini (MOAT) pamoj na kituo cha habari kwa wananchi TCIB na kudhaminiwa na Shirika la UNESCO.

Picha juu na chini baadhi ya washiriki wakifuatilia kongamano hilo sanjari na hotuba ya mgeni rasmi.

Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen akitoa Ujumbe wa Pamoja wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi  na Utamaduni (UNESCO) Irina Bokovas kuhusiana na Siku ya Uhuru wa Habari Duniani ulioenda sambamba na Kongamano la Uhuru wa vyombo vya Habari katika nchini za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene (kushoto) akiwa na wadau pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mh. Lennarth HJELMAKER (kulia) aliyeambata na mkewe katika kongamano hilo.

Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi akiwa na mtoto wa mwisho wa marehemu katika Kongamano hilo.

Pichani ni mmoja wa washiriki akionyesha bango lililokuwa na tukio la kuuwawa kwa Mwandishi wa Daudi Mwangosi ambalo limeandikwa” HABARI NI MUHIMU KATIKA UJENZI WA TAIFA, UKIMUUA MWANDISHI  WA HABARI UMEUA DEMOKRASIA, HAKI NA MAENDELEO YA NCHI YAKO”.

Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,  Dk. Richard Sezibera akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni 5 kwa Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi, Bi. Itika Mwangosi iliyotolewa na Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kumsaidia kuendesha maisha yake.

Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dk. Richard Sezibera na Mwenyekiti wa UTPC Tanzania Bw. Abubakari Karsani (kulia) kwa pamoja wakimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 5 Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi.

Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dk. Richard Sezibera akizungumza na mtoto wa mwisho wa Marehemu, Daudi Mwangosi mara baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 5 kwa mjane wa marehemu.

Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin kutoka UNESCO akifuatilia mada mbalimbali wakati wa kongamano hilo la Uhuru wa vyombo vya  Habari Duniani.

Mama Rahma wa Ofisi za Unesco Tanzania na Usia Nkhoma wa UNIC Dar.

Msanii wa kughani mashairi Mrisho Mpoto akitoa ujumbe wa waandishi wa habari kwenye siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari mbele ya mgeni rasmi na viongozi mbalimbali wa mashirika ya umoja wa mataifa na Serikali.

Mgeni rasmi akimfungua plasta mdomoni mmoja wa wasanii wa Band ya Mrisho Mpoto kama ishara ya kuwapa uhuru waandishi wa habari kuzungumza kilio chao mbele ya mgeni rasmi kama ujumbe wa siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani.

Wasanii wa Mrisho Mpoto wakiimba kwa hisia kali kuelezea madhila wayapatayo waandishi wa habari wawapo kazini ikiwemo usalama wao katika kazi zao za kila siku.

Mzee Kassim Mapili akiongoza Band ya Mrisho Mpoto kutoa burudani mara baada ya kongamano hilo kufunguliwa.

Mkurugenzi wa Habari-Maelezo Bw.Assah Mwambene (kushoto) akisalimiana na Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera.

Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dk. Richard Sezibera akiteta jambo na Balozi wa Sweden nchini Mh. Lennarth HJELMAKER nje ya ukumbi wa mikutano wa Kilamanjaro katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha.

Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera akiagana na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen ambao ndio wafadhili wa Kongamano hilo.

Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa  Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi Stella Vuzo (katikati) akiagana na  Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera mara baada ya kuzindua Kongomano la wahariri wa vyombo vya habari pamoja na waandishi ikiwa ni mwendelezo wa sherehe za Siku ya kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya  habari ulimwenguni.

Maveretans wa Tasnia ya Habari wakiwa na Mkurugenzi wa Misa Tan Tumaini Mwailege ( wa tatu kushoto) na Wa kwanza Kushoto ni Mama Eda Sanga, Mama Rosemary Haji wa UNESCO, Leila Shekha na Theophil Makunga wakifurahi baada ya kukutana katika Kongamano hilo.

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wakongwe katika tasnia ya Habari walioshiriki katika Kongamano hilo.