KANISA moja la Kianglikana nchini Uingereza limemuapisha mwanamke wa kwanza kuwa kasisi. Mchungaji Libby Lane ameapishwa katika sherehe iliofanyika eneo la York Minster, na atakuwa Kasisi wa Stockport ikiwa ni miezi sita tu baada ya kanisa hilo kumpigia kura ili kumaliza utamaduni wake wa wanaume kuwa makasisi.
Kasisi huyo alisema kuwa iwapo uchaguzi wake utawafanya wanawake kubaini uwezo wao basi anafurahia. Hatua hiyo imeendelea kuzua hisia tofauti miongoni mwa wafuasi wa kanisa hilo la kianglikana duniani.
Wakati huo huo; Watoto wawili wa aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak wameachiliwa huru kutoka jela, ikiwa ni miaka minne baada ya kukamatwa na kuzuiliwa kwa pamoja na baba yao.
wakuu wa Gereza wanasema kuwa Gamal na Alaa Mubarak wote wanabiashara maarufu waliachiliwa mapema leo Jumatatu. Juma lililopita mahakama iliamuru kuachiliwa kwao huku kesi dhidi yao kuhusu ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, ikiendelea. Mubarak anaendelea kuzuiliwa katika Hospitali moja ya kijeshi, ambapo anatumikia hukumu ya matumizi mabaya ya pesa za umma.
-BBC