Kaseja Akumbukwa Soka la Ufukweni

juma-kaseja-mbeya

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Ufukweni, John Mwansasu amemuita Kipa wa Mbeya City ya Mbeya, Juma Kaseja Juma kuongeza nguvu kwenye kikosi chake kinachotajia kusafiri kwenda Abidjan kucheza na wapinzani wao Ivory Coast kwenye mchezo wa marudiano wa kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kaseja mwenyewe, amefurahia wito huo na wakati wowote anatajiwa kujiunga na kambi hiyo iliyopo kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mwansasu amesema kwamba Kaseja anaweza kumsaidia kwenye kikosi chake kwa kuwa mbiu za mchezo huo, nafasi ya kipa inaweza kuamua matokeo kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza timu ya mafanikio hivyo amemuita kwenda kusaidiana na Ahamed Rajab.

Nyota wengine wanaounda kikosi hicho ni Talib Ame, Ahamada Ahamd, Mohammed Makame, Ahamed Rajab (golikipa) Khamis Said, Yacob Mohamed Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma Juma na Kevin Baraka.

Tanzania inatarajiwa kuondoka Septemba 14, mwaka huu kwenda jijini Abidjan, Ivory Coast ambako timu hizo zinacheza mchezo huo wa mwisho huko Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.

Itakumbukwa kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Agosti 26, 2016 hapa Dar es Salaam, Tanzania ililala kwa mabao 7-3 katika mchezo ambao ulichezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni Shafic Mugerwa atakayepuliza kipyenga na wasaidizi wake ni Ivan Bayige Kintu na Muhammad Ssenteza wakati Mtunza muda alikuwa Adil Ouchker wa Morocco na Kamishna akiwa ni Reverien Ndikuriyo wa Burundi.