Mwenyekiti wa Kariakoo Family Foundation (KFF) Mohamed Bhinda akiongoza kikao cha Kamati ya Utendaji katika kuandaa rasimu ya katiba ya chama hicho kinachotarajiwa kusajiliwa hivi karibuni kama taasisi isiyo ya kiserikali kwa nia ya kukutanisha upya wadau wote waliozaliwa, walioishi na wenye asili ya Kariakoo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam. Mkutano huu umefanyika leo jioni Kinondoni Studio. Kulia kwa Bhinda ni katibu wa chama hicho Senpai Wahid
Mtunza hazina wa KFF Yahaya Sameja akielezea namna chama hicho cha jamii ya wana Kariakoo kitavyoweza kujiendesha kwa njia za ada, michango na misaada ya wafadhili katika kuendeleza wanachama, ikiwa ni pamoja na kusaidiana katika shida na raha. Kushoto ni Mwenyekiti wa KFF Mohamed Bhinda na kati ni Makamu Mwenyekiti Tatu Lumelezi
Wana KFF wakipata mlo wa mchana wakati wa mapumziko
Jopo la kamati ya utendaji ya KFF baada ya mkutano wao leo