DENI la zaidi ya milioni 100 linalodaiwa Kanisa la Sinza Christian Center la jijini Dar es Salaam limesababisha kutupiwa nje vyombo vyake na dalali aliyepewa tenda hiyo na mahakama na mmiliki jengo hilo, Bw. Prosper Rwendera. Akizungumzia tukio hilo mke wa mmiliki wa jengo hilo, Bi. Patricia Prosper alisema; “huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu.”
Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa walipoulizwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.
Hili ni eneo la Kanisa hilo.
Viti vyote vikiwa vimetolewa nje ya kanisa hilo.
Baadhi ya vyombo vya muziki vya Kanisa la Sinza Christian Center la jijini Dar es Salaam vikiwa nje.
Magari yakiwa yanatolewa nje
Vitu vikiwa nje ya Jengo hilo ambapo mpaka sasa kuna sinto fahamu vinapelekwa wapi.
Vikombe nje.
Wametoa vitu vyote.
Magodoro na vitanda vyote nje.
Baadhi ya Magari yaliyotolewa katika Jengo hilo ambapo hapo awali ilikuwa ni Kanisa.
Kushoto kwa mbali ni Mke wa Miiliki wa Jengo hilo Bi. Patricia Prosper akiendelea na majukumu huku pembeni vijana wakipata maelekezo ya kuendelea kutoa vitu nje ya Jengo hilo. Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa