Kanisa la Anglikana Lapata Askofu Mkuu Ulimwenguni

Askofu Mkuu Mpya wa Kanisa la Anglikana Ulimwenguni, Justin Welby

KIONGOZI wa kiroho wa Kanisa la Anglikana, Justin Welby amesema ameshangazwa na nyadhifa aliyopewa ya Askofu Mkuu wa Kanisa Hilo Ulimwenguni ikiwa ni baada ya kuachia ngazi aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Rowan Williams. Askofu Welby alitoa kauli hiyo baada ya kuthibitishwa kwa nafasi yake hiyo mpya.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Askofu Justin Welby ambaye ni askofu wa Durham, alielezea msimamo wake wa kuunga mkono kutawazwa kwa wanawake kama maaskofu. Aliongeza kuwa watu watu hawapaswi kuwanyanyapa wapenzi wa jinsia moja kanisani, lakini akakiri kuna mgawanyiko kanisani kuhusu ndoa za jinsia moja.

Welby aliyefanya kazi katika sekta ya mafuta, anaonekana mhafidhina kwa mrengo wa kanisa hilo ambalo linaegemea upande wa Kiivanjelisti. Kiongozi huyo ataanza kazi mwezi Machi mwaka ujao baada ya Askfo Mkuu Rowan Williams kuachia ngazi. Baada ya uteuzi wa Askofu Mkuu Justin Welby kuwa Mkuu wa Kanisa la Anglikana, viongozi mbalimbali wa kanisa hilo wamezungumzia uteuzi huo.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini Nigeria, Nichola Okoh, amesema kuwa uhusiano wa wapenzi wa jinsia moja usitetewe na Kanisa.

-BBC