NA MAGRETH KINABO
ELIMU ya uzalendo imesaidia kuwafanya vijana wa Kitanzania kuipenda nchi yao , hali iliyochangia nchi yetu kuwa na amani na utulivu.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo,Seth Kamuhanda wakati akizungumza na ujumbe wa watu 22,baadhi yao ni viongozi wa utawala na 13 ni wanafunzi wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu wa mafunzo ya kijeshi kutoka Nigeria.
Ujumbe huo umetembelea wizara hiyo kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ya Utamaduni wa Kitanzania, umeongozwa na kiongozi wa msafara, Meja Generali, Ati John,ambaye ni Mkurugenzi wa Jeshi la Wanamaji.
“Mojawapo ya program tunazowafundisha vijana ili kuondoa migogoro katika nchi yetu ni elimu ya uzalendo ,yaani tunawafundisha jinsi ya kuipenda nchi yao. Elimu hii imesaidia kupunguza migogoro,alisema.” Katibu Mkuu huyo alipokuwa akijibu swali la mmoja ya wanafunzi hao lililouliza kuwa kuna program zipi zinazochangia kupunguza migogoro hususan kwa vijana.
Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa kuna mkakati wa kuwawezesha vijana kiuchumi ili waweze kubuni miradi mbalimbali kwa kuwa na mfuko wa vijana.
Alisema katika mpango huo vijana wanakuwa katika vikundi na kufanya shughuli mbalimbali kuwawezesha kiuchumi.
Aidha Katibu Mkuu huyo akizungumza kuhusu masuala ya kiutamaduni ,alisema wizara yake ndi yenye jukumu lakuendeleza Utamaduni wa Mtanzania, hivyo katikawizara hiyo yenye sekta nne, ambazo ni Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Kamuhanda alisema sektaya utamuduni ndio inayofanyakazi ya kudumisha Utamaduni huo.
Aliongeza kuwa lugha ya Kiswahili ndio imekuwa lugha kuu ya mawasiliano nchini na ndiyo iliyoleta umoja ,amani na mshikamano.
Wakizungumzia kuhusu ziara hiyo kiongozi huyo na mmoja wa wanafunzi, Ikema Francis walisema wameshukuru kwa taarifa walizopata kuhusu wa masuala hayo ya kiutamaduni na kuhafamu kuwa lugha ya Kiswahili ndiyo imeleta umoja.