Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Kulia ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Tanzania, Bruth Zhang (kushoto) wakishuhudia.
|
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (katikati) akipiga makofi pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Tanzania, Bruth Zhang (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano.
|
|
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. |
|
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora akizungumza kabla ya kuzinduwa rasmi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. |
|
Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Peter Ngota akizungumza katika uzinduzi wa teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. |
|
Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Tanzania, Bruth Zhang akizungumza katika uzinduzi wa teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni hiyo ambayo ni mshirika wa Kampuni ya TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. |
|
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (mwenye suti ya kijivu) akizunguka kupata maelezo namna teknolojia ya 4.5G inayofanya kazi wengine ni viongozi waandamizi wa Kampuni ya Huawei na TTCL. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. |
|
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (mwenye suti ya kijivu) akizunguka kupata maelezo namna teknolojia ya 4.5G inayofanya kazi wengine ni viongozi waandamizi wa Kampuni ya Huawei na TTCL. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. |
|
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (mwenye suti ya kijivu) akizunguka kupata maelezo namna teknolojia ya 4.5G inayofanya kazi wengine ni viongozi waandamizi wa Kampuni ya Huawei na TTCL. Kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Meza kuu ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (mwenye suti ya kijivu) ikipata maelezo namna teknolojia ya 4.5G inayofanya kazi wengine ni viongozi waandamizi wa Kampuni ya Huawei na TTCL. |
|
Kulia mmoja wa wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano akicheza gemu kwa kutumia teknolojia hiyo. |
|
Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Peter Ngota (kulia) akipongezwa na baadhi ya wageni waalikwa mara baada ya kampuni ya TTCL kwa kushirikiana na Huawei kuzinduwa teknolojia ya 4.5G jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. |
|
|
|
|
|
|
|
AWALI akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba alisema uzinduzi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G unaifanya TTCL kuwa Kampuni ya kwanza nchini na eneo lote la Afrika Mashariki kutoa huduma yenye kiwango cha juu kabisa cha kasi na ubora katika huduma za Intaneti.
Alisema TTCL inaendelea kutekeleza mpango wa mageuzi ya kibiashara ambapo hatua mbali mbali zinachukuliwa katika kuboresha huduma zake. Hatua zinazochukuliwa zinalenga katika kuirejesha Kampuni katika hadhi yake ya kuwa Mhimili mkuu wa Mawasiliano nchini, kiungo muhimu cha kufanikisha shughuli za ukuaji wa sekta nyingine na mchangiaji muhimu katika Pato la Taifa.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora akizungumza katikauzinduzi huo alisema, Serikali imepokea taarifa ya uzinduzi wa 4.5G kwa furaha kubwa na kuamini kuwa sasa, TTCL ambayo ni mhimili mkuu wa Mawasiliano nchini inafanya kile ambacho Taifa zima lilitegemea kupata kutoka kwa Kampuni hii.
“…Naipongeza Menejimenti na Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa juhudi kubwa za kuleta mabadiliko ya utendaji na uwajibikaji, ambao ni utekelezaji wa mwongozo wa Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais mpendwa Mhe Dkt John Pombe Magufuli,” alisema Profesa Faustine Kamuzora.