Kampuni ya Tigo Yatoa Madawati 400 Shule za Msingi Morogoro

Mkurugenzi wa tigo kanda ya pwani Goodluck Charles akimkabidhi Afisa wa Elimu wilaya ya Morogoro vijijini Donald Pambe msaada wa madawati 400 katika shule 10 za wilaya hiyo hafla iliyofanyika katika shule ya msingi  Kibangile

Mkurugenzi wa tigo kanda ya pwani Goodluck Charles akimkabidhi Afisa wa Elimu wilaya ya Morogoro vijijini Donald Pambe msaada wa madawati 400 katika shule 10 za wilaya hiyo hafla iliyofanyika katika shule ya msingi  Kibangile

 

Mbunge wa jimbo la Morogoro kusini Prosper Mbena akimshukuru Mkurugenzi wa tigo kanda ya pwani  Goodluck Charles baada ya hafla ya kukabidhi  msaada wa madawati 400 yaliyotolewa na kampuni ya Tigo Tanzania kwa  shule 10 za jimbo la morogoro kusini.

Mkurugenzi wa Tigo, kanda ya Pwani Goodluck Charles(wa nyuma kushoto) na Afisa  Uhusiano wa Tigo Halima Okash (mbele kushoto) wakikabidhi madawati 400 yaliyotolea na kampuni ya tigo Tanzania kwa shule kumi za wilaya ya Morogoro vijijini kwa mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mh Prosper Mbena (nyuma kulia) na Afisa Elimu wilaya hiyo Donald Pambe katika shule ya msingi Kibangile iliyopo kata ya Matombo.

KAPUNI ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 60 kwenye shule 10 za msingi katika mkoa wa Morogoro ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Msingi Kibangile iliyopo Kitemu katika kata ya Matambo, Morogoro Kusini, Mkurugenzi wa Tigo wa Kanda ya Pwani Goodluck Charles mchango huo ni sehemu ya utekelzaji dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.
“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, “alisema Charles.
Charles alisema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya na Iringa na kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini siku za zijazo.
Makabidhiano yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dr Rajabu Rutengwe ambaye alisema madawati hayo 400 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Mporogoro na kutoa wito kwa wadahu wengine kuunga mkono zoezi hilo.
“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la ukosefu wa
madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa Morogoro. Ni Dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 400 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao katika mazingira bora Zaidi,” alisema Dr Rutengwe.