*Zaidi ya milioni 700 Kushindaniwa Kupitia Bia ya Serengeti
KATIKA mpango mwingine wa kutambua thamani ya wateja, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imezindua kampeni ya kufaidisha wateja ambapo baadhi ya wateja watashinda safari iliyolipiwa kwenda nchini Brazil, hii ikiwa ni moja kati ya zawadi nyingi nyingine zitakazoshindaniwa. Kampeni hii imeanza tayari na itaendelea kwa muda wa kipindi cha miezi mitatu wateja kujishindia.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na wanahabari, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru alisema wateja wanaweza kushiriki mara nyingi watakavyoweza huku kukiwa na zawadi za fedha shs milioni 100 zitakazotolewa kwa wateja watakaoshinda. Alisema mteja anaweza kujishindia kuanzia kiasi cha shs 5,000 hadi shs 10,000 na bia ya bure ambayo mtu atashinda papo hapo.
Akifafanua zaidi alisema mtumiaji atakapofungua bia ya Serengeti, chini ya kizibo atakuta namba ambazo atazituma kwenda namba 15317 na papo hapo zawadi itaonyeswa kwenye ujumbe mfupi atakaopokea. “…Kampeni hii kama kampeni za hapo awali, itakuwa inasimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Washirika wengine ambao watakuwa wanahakiki uaminifu wa zoezi zima ni PWC na Push mobile,” alisema Mafuru.
Uzinduzi huo uliofanyika katika kiwanda cha Bia cha Serengeti Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa Masoko, Mafuru pia aliongeza kuwa promosheni hiyo si tu kwa ajili ya kuongeza mauzo ya bidhaa yao lakini bali kuwatunuku wateja kwa kupendelea bidhaa za SBL.
“Katika shughuli zetu zote, tunapenda kuwa karibu sana na jamii inayotuzunguka. Tunajaribu kuangalia kwa makini na kujua mahitaji yao. Ingawa hatuwezi kushughulikia mahitaji yote wanayohitaji, tunahakikisha chochote tunachofanya kinagusa maisha ya wateja wetu. Tunashiriki katika shughuli mbalimbali ambazo zitaboresha maisha ya kila raia. Kuanzia mipango ya kijamii mpaka shughuli zinazohusu bidhaa zetu, kama hii iliyotuleta hapa leo,” alisema Mafuru.
Aidha, SBL imeanzisha promosheni mapema katika mwaka 2014 kwa kuwa kuna shughuli nyingi zimepangwa mbeleni mwaka huu zote zikilenga kuwashukuru na kuwaonesha dhamana wateja wake. Aliongeza kuwa watumiaji wa bia ya Serengeti wamecheza nafasi kubwa sana katika ukuaji wa bidhaa hiyo ambao ni wa kasi. Pia ilijizolea tuzo za DLG za ubora wa bidhaa mara tatu na imekuwa moja kati ya bia zinazokubalika zaidi nchini kwa ubora.
“Tunashuhudia promosheni nyingi kwenye soko letu, na zote zikiwa na nia ya kuongeza mauzo bila kujali nini kinashindaniwa. Hiyo ni tofauti kwa kampuni ya bia ya Serengeti, kwetu sisi zawadi ni ile itakayogusa na kubadili maisha ya mshindi kwa mtazamo chanya. Zawadi yetu kubwa itakuwa safari ya Brazil ambayo washindi wetu watapata uzoefu wa kusafiri daraja la kwanza na kukaa Brazil huku gharama zote zikilipiwa, kwa washindi wetu itakuwa ni safari isiyosahaulika “. Aliongeza Bw. Mafuru.
Naye, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Allan Chonjo akifafanua zaidi alisema kwa sasa SBL imejipanga na wateja hawata pata kikwazo chochote katika kupata zawadi zao. “…Nirahisi tu we nunua chupa ya bia ya Serengeti, angalia chini ya kizibo, ukipata picha ya bia ina maana unapata bia ya bure na unaichukua papo hapo. Ukipata tarakimu 6 za kipekee, unazituma kupitia ujumbe mfupi wa tarakimu hizo kwenda nambari 15317 na utapata ujumbe papo hapo wenye majibu yafuatayo: kwamba umeshinda, umekuwa mshindi wa fedha taslimu kati ya shs 5,000 na shs 10,000 , ambayo mteja atatumiwa kupitia M-Pesa au atapata ujumbe mfupi kushukuru kwa kushiriki na kutamtaka kuendelea kushiriki,” alisema Chonjo.
Aidha alisema kwa mteja kushiriki tu atakuwa ameingia kwenye droo ambayo unaweza kujishindia safari ya brazil, king’amuzi cha Azam na Ipad. Hata hivyo gharama za kutuma ujumbe mfupi katika shindano hilo ni sawa na gharama ya kutuma ujumbe wa kawaida na unaweza kushiriki kupitia mtandao wowote. Safari ya Brazil itakuwa kati ya mwezi wa sita na saba mwaka 2014. Kwa maelezo zaidi fuatilia ukurasa wa kijamii wa facebook wa bia ya Serengeti.
Kunywa kwa tahadhari. Inauzwa kwa wenye miaka 18+, Kampuni ya bia ya Serengeti ni kampuni tanzu ya kampuni ya EABL/ DIAGEO.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano, Evans Mlewa evans.mlewa@diageo.com; Simu +255 784 990440 au tembelea tovuti ya DrinkQ.com