Waandishi wa habari wa mkoani Dodoma wakichukua matukio wakati wa mkutano uliofanyika mapema jana katika hoteli ya Morena mkoani Dodoma.
|
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti imewapatia Watanzania zaidi ya milioni mbili kote nchini maji safi na salama bure katika kipindi cha miaka sita iliyopita kupitia programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo inayolenga kuboresha maisha.
“SBL ina sera iliyojikita katika ustawi wa jamii yetu ambapo Maji ya Maisha ikiwa ni moja ya maeneo manne ya kipaumbele ambayo kampuni yetu imeyafafanua katika malengo yake ya kutoa msaada kijamii kwa jamii inamofanya shughuli zake, alisema Wanyancha akifafanua maeneo mengine ya kipaumbele kama Kutoa Stadi za Maisha, Mazingira Endelevu na Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.
Wanyancha aliongeza kwamba kwa kutoa huduma ya maji ya uhakika katika jamii, SBL imewawezesha watu kutumia muda mwingi zaidi katika uzalishaji kuliko kusafiri umbali mrefu kutafuta maji.
Aliongeza, “licha ya kuboresha afya za wakazi wa maeneo hayo, upatikanaji wa maji safi na salama ndani ya jamii unahakikisha kuwa watoto hususani watoto wa kike wanaosoma shule wanapata muda mzuri wa kuhudhuria shuleni kwa uhuru zaidi bila usumbufu”.
Mkurugenzi huyo wa Mahusiano alieleza kwamba mpango wa Maji ya Maisha kwa mwaka 2017 ni kuanzisha miradi zaidi katika maeneo ya Ngare Nairobi, wilayani Siha, Chang’ombe B wilayani Temeke (Dar es Salaam) na Karatu na Likamba katika mkoa wa Arusha ambapo miradi yote itawanufaisha wakazi zaidi ya 300,000.