Mgombea wa CCM Jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari akiomba kura mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni za CCM katika Mji mdogo wa Mbuguni, Kata ya Mbuguni.
Meneja kampeni za CCM, uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha CCM, Mwigulu Nchemba (kulia) akimnadi mgombea wa CCM jimbo hilo, Sioi Sumari katika mkutano wa kampeni uliofanyika Machi 14, 2012 katika kijiji cha Shambarai, Kata ya Mbuguni.(Picha na Bashir Nkoromo)
Malikia wa mipasho Khadija Omari Kopa na wasanii wenake wa kundi la Tanzania One Thetre (TOT) wakishambulia jukwaa kwenye mkutano wa Mji mdogo wa Mbuguni, Arumeru Mashariki.
Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa mji mdogo wa Mbuguni Kata ya Mbuguni.