Mmoja wa vijana wahamasishaji na mcheza Ngoma akitoa maelezo ya Elimu ya Chakula na Lishe bora kwa wafanyabishara na wananchi mbalimbali waliohudhuria kampeni ya Ulaji unaofaa kwa Afya yako iliyoendeshwa na shirika la Chakula Duniani (WFP).
Mmoja wa wanakikundi cha Ngoma cha Uhamasishaji akigawa vipeperushi vyenye ujumbe wa Chakula na Lishe bora kwa baadhi ya wafanyabiashara na wananchi katika Soko la Mabibo jijini Dar leo.
Baadhi ya wafanyabiashara na wananchi wakisoma vipeperushi vya Chakula na Lishe bora vilivyosambazwa na WFP ikiwa ni kampeni ya Ulaji unaofaa kwa Afya yako.
Baadhi ya Wafanyabaisha wa Soko la Mabibo na Wananchi wakifuatilia burudani ya Ngoma iliyokuwa ikitumbuiza kwa njia ya sanaa kuhamasisha Umuhimu wa Chakula na Lishe bora kwa jamii.
Baadhi ya wacheza ngoma wakiwaburudisha wafanyabiashara katika soko la Mabibo huku wakitoa Elimu ya umuhimu wa Chakula na Lishe bora kwa jamii.
Mmoja wa wafanyabiashara wa Soko la Mabibo Latifa Mbwambo akizungumza na waandishi wa habari umuhimu wa kuwa na chakula na lishe bora kuanzia ngazi ya familia hadi taifa ambapo pia amelishukuru shirika la Chakula duniani (WFP) kwa kuhamasisha jamii umuhimu Lishe Bora kwa Afya.
Mkazi wa Dar es Salaam Mzee Yakubu Salum akizungumza na wanahabari jinsi kampeni hiyo ya Lishe Bora ilivyona manufaa kwa jamii.
Kikundi cha Uhamasishaji kilichotumika kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu Lishe Bora kuanzia ngazi ya Familia mpaka Taifa.
Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mabibo wakisubiria wateja.
Mishemishe zikiendelea kwenye soko la Mabibo jijini Dar.
Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika na utapiamlo 42% ya watoto chini miaka 5 wamedumaa
*asilimia 16 ya watoto wana uzito pungufu nchini
Na Moblog Team
SHIRIKA LA CHAKULA DUNIANI (WFP) Tanzania, Kwa kushirikiana Na Shirika la Chakula Na Kituo cha Lishe Tanzania (TFNC) Na MuDA Africa, wafanya kampeni maalum ya elimu iliyoambata na ngoma katika kuelimisha umma umuhimu wa chakula bora kwa ajili ya afya ya jamii jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari katika soko la mabibo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mahusiano wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Fizza Moloo amesema kwamba shirika hilo limeamua kuendesha kampeni hiyo iliyoambatana na ngoma za asili ili kuelimisha jamii umuhimu wa chakula bora na lishe sahihi kwa ajili ya kulinda afya ya watumiaji.
“tumemua kuwa na kampeni hii ya elimu juu ya chakula bora kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ili kupitia hadhara hii basi elimu hii ya chakula na lishe bora iweze kufika maeneo yote nchi nzima mpaka mikoani,’ amesema Moloo.
Moloo amesema kwamba wameamua kutumia njia ya ngoma kwa vijana kucheza katika kurahisisha kupeleka ujumbe huu mahusus kwa jamii ili wananchi waweze kupata elimu sahihi juu ya lishe bora kwa afya ya mtu moja moja na jamii kwa ujumla.
Amesema kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika sana na utapiamlo katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara ikiwa na asilimia 42 ya watoto chini ya miaka 5 wamedumaa na asilimia 16 wana uzito pungufu.
Moloo alifafanua kwamba watoto sita kati ya kumi wenye umri kati ya miezi 6-59 wana upungufu wa wekundu wa damu (DHS, 2010), amesema lishe duni ni tatizo kubwa kwa wanawake walio kwenye umri wa kuzaa, wakati zaidi ya nusu ya wanawake wajawazito wana upungufu wa damu.
Amesema Mpango wa Chakula duniani umedhamiria kuisaidia Serikali ya Tanzania kufikia malengo yanayohusiana na lishe kwa mujibu wa Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini Tanzania (MKUKUTA 11) na Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Lishe (2011-2016).
Kwa upande wao, mmoja wa wafanyabiashara wa soko la mabibo, Ratifa Mbwambo amesema wanalishukuru shirika la Chakula duniani kwa kuhamasisha jamii umuhimu wa kuwa na chakula na lishe bora kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
“kwa kweli tunawashukuru sana kwa kuja katika soko letu la mabibo na kuelimisha watu umuhimu wa chakula bora kwa njia ya kupangilia mlo sahihi kwa kila siku,” amesema.
Amesema ni muhimu kwa shirika hilo kufanya kampeni za namna hii mara kwa mara katika kuikumbusha jamii umuhimu wa kuzingatia lishe bora kwa kulinda afya ya jamii nzima kwa ujumla na vile vile elimu iendelee kutolewa ili watu wajifunze kadri iwezekanavyo.