Mkurungezi wa Kampuni ya MSAMA PROMOTION, Alex Msama pichani mwenye fulana akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) CD za video na Audio za muziki wa aina mbalimbali pamoja na kompyuta za kudurufu kazi za wasanii kwa njia ya wizi kwenye kituo kikuu cha Polisi mkoani Dodoma, mara baada ya kukamilisha zoezi la kusaka na kuwakamata wezi wa kazi za wasanii, ambapo jumla ya CD na komputer zenye thamani ya sh. milioni 67 zilikamatwa kwa msaada wa Jeshi la Polisi mkoani humo. (PICHA ZOTE NA DIRA MEDIA).