TAARIFA ambazo mtandao huu umezipata kutoka ndani ya Jeshi la Polisi ni kwamba Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow ameuawa kwa risasi usiku wa kuamkia leo na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi.
Taarifa hizi zimethibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP, Said Mwema. Inadaiwa kuwa tukio lilitokea katika eneo la Kitangiri usiku wa saa saba ambapo kiongozi huyo alikuwa akimrudisha nyumbani mmoja wa dada zake ambaye walikuwa naye katika kikao cha harusi. Mtandao huu unafuatilia na taarifa zaidi zitatolewa.