JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) leo limetimiza Miaka 50 toka Kuanzishwa kwake mnamo tarehe 1/09/1964. JWTZ ni moja ya Jeshi lililotajwa na Mtandao mmoja hivi karibuni kuwa ni Jeshi lenye weredi wa hali juu Duniani kutokana na Operesheni ambazo wamewahi kuzifanya na linalotumia Silaha za Kisasa. Baadhi ya Operesheni zilizowahi kufanywa na Jeshi la Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) ni Ile ya Kuwasambaratisha Waasi Wa M23 nchini Congo, Operesheni ya Comoro, Operesheni nyingine ni Ile ya Kulinda Amani Sudan wakiwa wameungana na Majeshi Mengine Kutoka Umoja wa Mataifa (UN)
Jeshi la Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) limejipatia Umaarufu na sifa kutokana na Kuwa na Askari wenye Nidhamu ya Hali ya Juu na Kuwachukulia Hatua kwa Haraka Askari wake ambao wameonyesha utovu wa Nidhamu kwa Wananchi na Jamii kwa Ujumla lakini Pia Sifa Hiyo Kubwa Imekuja Kutokana na uwezo mkubwa wa Kivita na Kuweza Kuwasambaratisha Waasi wa Kikundi cha M23 nchini Congo.
Jukumu kubwa la Kazi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya Wavamizi na Vile vile Kushiriki katika kulinda Amani Katika Ngazi ya Kimataifa lakini Pia Pamoja na Majukumu hayo vilevile Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa Mstari wa Mbele katika Kujitoa kwenye shughuli za Kijamii kama Vile Matibabu, Elimu nk na Wamekuwa Mstari wa Mbele katika Kusaidia Jamii katika shughuli mbalimbali kama Vile za Uokoaji katika Maafa yanayotokea Nchini.
Kwa kifupi Sahivi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa jeshi la Kisasa na wasomi ambao wanalisaidia Jeshi katika Kufanikisha Malengo yake kama Kulinda Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kujitoa katika shughuli nyingine za kijamii. Hongera ya Kutimiza Miaka 50 Tokea Kuanzishwa.
Chanzo: Lukaza Blog