JUVE YAISAMBARATISHA LAZIO

Baada ya kuanza vibaya katika msimu wa ligi ya Italia, timu ya Juventus ambayo ipo nafasi ya nne, kocha wao anasisitiza hawawezi kuchukua ubingwa kwa matokeo kama hayo wasipofanya juhudi.

Kocha wa klabu hiyo Massimiliano Allegri amesisitiza Juventus lazima kuwa wanyenyekevu na kuendelea kuboresha kikosi kama wanahitaji kuwa mabingwa msimu huu kufuatia ushindi walioupata jana dhidi ya Lazio wa bao 2-0.

bao la Kujifunga kutoka Santiago Gentiletti na kisha Paulo Dybala kugongelea msumari wa mwisho ulitosha kuwasaidia Juve kuweka historia ya kushinda michezo mitano mfululizo.

“Haikuwa rahisi kushinda mchezo huu, ili tulikuwa na kila sababu ya kuongeza juhudi ili tushinde mchezo huu” alisema.

“Ilikuwa lazima tuoneshe ubora, Lazio ni timu imara, hivyo tutaboresha nyanja za kiufundi tuweze kupata matokeo mazuri ziadi kwa michezo inayofuata

“Ligi bado ni ndefu na sisi pia tunacheza katika mashindano mengine. Kila mtu atakuwa na nafasi yake. Sisi si kuangalia wengine, lakini tu kuangalia nini tunafanya sisi wenyewe.

“Ilikuwa ni muhimu kwa kuja mbali na ushindi. Sisi tunamchezo mwingine katikati ya wiki, tunataka kuingia kwenye kumi bora katika Ligi ya Mabingwa.”

Juventus watasafiri kwenda kucheza na Sevilla Jumanne katika mchezo wa kundi D.