Jumuia ya Wazazi CCM Arusha Wasaidia Mahabusu ya Watoto

Mjumbe wa kamati ya Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Arusha, Phidesia Mwakitalima akiwa anatandika moja ya mashuka waliyotoa kama msaada katika mahabusu ya watoto Jiji la Arusha wakati alipotembelea mahabusu hiyo.

Mjumbe wa kamati ya Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Arusha, Phidesia Mwakitalima akiwa anatandika moja ya mashuka waliyotoa kama msaada katika mahabusu ya watoto Jiji la Arusha wakati alipotembelea mahabusu hiyo.

Sehemu ya misaada iliyotolewa katika kituo hicho cha mahabusu ya watoto.

Sehemu ya misaada iliyotolewa katika kituo hicho cha mahabusu ya watoto.

Katibu wa Jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Arusha, Rehema Mohamed akiwa anamkabidhi Ofisa Ustawi wa Jamii Mahabusu ya watoto, Mussa Mkamate fyekeo kwa ajili ya kufyekea majani katika maeneo ya mahabusu.

Katibu wa Jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Arusha, Rehema Mohamed akiwa anamkabidhi Ofisa Ustawi wa Jamii Mahabusu ya watoto, Mussa Mkamate fyekeo kwa ajili ya kufyekea majani katika maeneo ya mahabusu.

Na Woinde Shizza, Arusha
 
SERIKALI imetakiwa kuangalia kwa makini mahabusu ya watoto ya mkoa wa Arusha kwani mahabusu hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ubovu wa majengo pamoja na ukosefu wa dawa na usafiri kwa ajili ya mahabusu hiyo.
 
Hayo yameelezwa juzi na baadhi ya wajumbe wakamati ya utekelezaji Jumuia ya wazazi wilaya ya Arusha wakati walipotembelea na kutoa msaada katika mahabusu hiyo ya watoto ilipo ndani ya jiji la Arusha.
 
Kwa upande wake katibu wa Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Arusha, Rehema Mohamed aliitaka serikali kuangalia kwa makini sana mahabusu hiyo kwani watoto wanaoishi katika mahabusu hiyo wamekuwa wanateseka sana kutokana na mazingira ya mahabusu hiyo.
 
Aidha aliitaka pia mahakama kujitaidi kusikiliza kesi za watoto hao kwani wengi wao wamekaa kwa kipindi cha mda mrefu bila kesi zao kusikilizwa na badala yake wamekuwa wakiambiwa kila siku upelelezi haujakamilika.
 
Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya Jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Arusha, Phidesia Mwakitalima ambaye pia ni mwanamke pekee ambaye alieweza kuwakilisha Mkoa wa Arusha katika kinyanganyiro cha kugombea ubunge wa wazazi
taifa. Alisema serikali inatakiwa kuangalia kwa makini mahabusu ya watoto kwani mbali na na changamoto zilizopo, mahabusu hiyo watoto wanapokuwa wagonjwa hupelekwa hospitali kwa pikipiki kwani hakuna gari ya mahabusu ilhali wakati mwingine dawa zinakosekana na maofisa kujikuta wakijipapasa mifukoni mwao kunusuru watoto umauti
usiwakute.

Alisema kuwa wao kama wazazi wamekuwa wanaumia sana kuona watoto hawa wakiteseka kwani watoto hawa wanayo haki kama vile watoto walioko nyumbani huku akiomba Halmashauri ya Jiji la Arusha kuwakumbuka watoto hawa hata kwa vyakula na matunda.
 
“..kuna haya matunda ambayo halmashauri ya jiji huwa wanayakamata kwa wafanya biashara ambao wanauza bidhaa zao sehemu ambazo si staili sasa napenda nitoe wito kwa mkurugenzi pamoja hata na mkuu wa mkoa iwapo wanakamata
matunda hayo na vyakula hivi wawaletee watoto hawa ili nao wakiwa huku ndani wakila wajisikie nao kama watoto waliopo majumbani,” alisema Phidesia.

Aidha alitumia nafasi hiyo kuiomba serikali isaidie kuleta walimu ambao wataweza kuwafundisha masomo mbalimbali yakiwemo ya ufudi, VETA ili pale ambapo kesi zao zitasikilizwa na hukumu kutolewa huku wengine wakiwa wamemaliza hukumu zao waweze kutoka na ujuzi ambao utawasaidia pale ambapo wataenda uraiani.

“Unajua wakipata elimu kuanzia huku hata akienda mtaani ataweza kujishirikisha na makundi mabovu au naweza kusema mabaya ambayo anaweza kukaanayo na kumfanya afanye uhalifu tena na badala yake ujuzi utamfanya aendelee kutengeneza vitu vyake vitakavyo muingizia kipato,” alisema Phidesia.

Kwa upande wake, Ofisa Ustawi wa Jamii Mahabusu ya Watoto Arusha, Mussa Mkamate alisema kuwa wanashukuru kwa msaada huo ambao wameletewa kwa sasa kwani utawasaidia kwa kiasi kikubwa huku akiwasihi wadau wengine kujitolea kwenda kutembelea watoto hao na mahabusu hiyo.
 
Alisema kuwa mahabusu hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambapo alizitaja changamoto hizo ni pamoja na tatizo la kukosa choo cha kutumia mahabusu hao kwani, mahabusu wamekuwa wakitumia choo kimoja na kutolea mfano wa mahabusu ya watoto wa kiume wapo 48 lakini wanatumia choo kimoja.