Jukwaa la Wazi Kujadili Athari za Ukeketaji

Bango linaloonesha ofisi za TGNP utakapofanyika mkutano huo


JUKWAA la wazi la Mfululizo wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS), linawaletea majadiliano ya wazi juu ya athari za Ukeketaji kwa wanawake na wasichana. Majadiliano yatafanyika Viwanja vya zilipo Ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Barabara ya Mabibo Karibu na Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji Mabibo Sokoni.

JUKWAA LA WAZI LA KIJAMII
KARIBU SEMINA ZA JINSIA NA MAENDELEO ZA KILA JUMA TANO
MADA: ATHARI ZA UKEKETAJI KWA WANAWAKE, WASICHA NA WATOTO 
LINI: Jumatano Tarehe 10/07/2013
MUDA: Saa 9:00 – 11:00 JIONI
WAPI:  Viwanja vya TGNP, Barabara ya Mabibo Karibu na Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji Mabibo Sokoni 
MTOA MADA: Judica Losai – TAMWA