JPM AIPONGEZA TTCL SABASABA, YAIBUKA KIDEDEA SEKTA YA MAWASILIANO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akimkabidhi tuzo ya Ushindi wa kwanza katika kundi la Watoa huduma za Mawasiliano na Tehama Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) alipokuwa akifungua rasmi maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage.

 

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (wa tatu kushoto) akipiga picha na maofisa mbalimbali wa TTCL pamoja na wageni waliotembelea Banda la TTCL kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono wananchi na maofisa na wafanyakazi wa TTCL mara baada ya kutembelea banda la Kampuni ya Simu Tanzania wakati akifungua rasmi maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

 

RAIS wao Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli, ameipongeza Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kwa juhudi kubwa inazofanya katika kuwapatia Wananchi huduma bora za Mawasiliano.

Rais Magufuli ametoa pongezi hizo baada ya kuitembelea Banda la TTCL katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

Rais Magufuli alifika katika Banda la TTCL mara baada ya kufungua rasmi maonesho hayo na kukabidhi zawadi kwa Washindi mbalimbali, ambapo Kampuni ya TTCL iliibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Watoa huduma za Mawasiliano na Tehama.

Katika Banda la Maonesho la TTCL, Rais Magufuli alipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhe Omari Nundu na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba ambao walimhakikishia Mhe Rais Magufuli kuwa kampuni hiyo inafanya mageuzi makubwa ya kibiashara yatakayoiwezesha kurejea katika nafasi yake ya kuwa Kinara wa Sekta hiyo nchini.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba alisema, TTCL inatarajia kuanza kutoa gawio Serikalini mwaka huu na kumuomba, Mhe Rais kuiongezea mtaji Kampuni hiyo ombi ambalo Mhe Rais alilipokea na kuahidi kulifanyia kazi.

 

Huduma mbalimbali zikitolewa kwa wanaichi wanaotembelea Banda la Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhe Omari Nundu alipowasili katika banda la Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, Sabasaba.

 

Huduma mbalimbali zikitolewa kwa wanaichi wanaotembelea Banda la Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.