JovagoTanzania- Hali ya Uchumi Dhidi ya Sekta ya Utalii,

MAPANGO YA AMBONI
Kutokana na mapitio ya kiuchumi yaliyofanyika na (B.O.T) Benki ya Tanzania, inaonyesha uchumi umeongezeka kutoka 5.1% kwa mwezi Mei mpaka 6.1% mwishoni mwa mwezi Juni 2015.

Hata hivyo, kutokana na ripoti iliyotolewa na Tanzania Investment (2015); Shilingi ya Kitanzania imepungua dhidi ya dola ya Kimarekani kwa 6.4% ambapo ni wastani wa shilingi ya Kitanzania 2,082.5 kulinganisha na mwezi Mei 2015 kwa shilingi 1,957.

Mr. Andrea Guzzoni Meneja mkazi wa kampuni ya Jovago Tanzania alifafanua kwamba, hali ya uchumi Tanzania haipo katika hatua mbaya iwapo juhudi za ufuatiliaji kwenye sekta mbalimbali zitatekelezeka ikiwemo kupunguza malipo kwa kutumia dola badala ya shillingi za Kitanzania, “kuhamisisha matumizi ya fedha zetu, itasaidia kupanda kwa thamani ya shilingi yetu” aliongezea.

“kwa upande mwingine inabidi kutambua kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi za kipekee ambayo zaidi ya 25% ya eneo la nchi ni hifadhi za Taifa”alifafanua.

Mr.Guzzoni, anafafanua kwamba, ongezeko la watalii bado ni chachu ya maendeleo Tanzania, ikiwa kwa mwaka tunapokea idadi kubwa ya watalii kutoka ndani na nje ya nchi; “Mwaka 1995 kulikuwa na idadi ya watalii 295,312 hadi kufikia 2014 watalii wameongezeka kufikia 1,140,156”.

Hivyo, kukua kwa uchumi wa Tanzania kunasababishwa haswa na sekta muhimu mbili ambazo ni sekta ya utalii na kilimo. Ongezeko la watalii Tanzania imechangia zaidi ya dola milioni 2,006.32 kwa mwaka 2014, ambapo pamoja na mauzo ya bidhaa asilia nje ya nchi zimekuwa ni vyanzo vikuu katika kuongeza pato la dola za kimarekani million 9,398.5 sawa na 9.4% mpaka kufikia june 2015, (Tanzania investment, 2015).

Kwa upande mwingine, sekta moja haiwezi kuleta mabadiliko ya kiuchumi; usafiri wa uhakika, afya na miundo mbinu inayoeleweka itapelekea kukuza sekta ya utalii na kutanuka kwa soko la nje ya nchi.