Jovago Tanzania Wazinduwa Wavuti ya Kiswahili

Meneja wa Jovago nchini Tanzania, Andrea Guzzoni (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wanahabari katika hafla fupi ya uzinduzi wavuti ya Kiswahili ya Jovago leo jijini Dar es Salaam.

WADAU wakubwa wa sekta ya utalii nchini Tanzania Kampuni ya Jovago Tanzania sasa imeingiza lugha ya Kiswahili katika matumizi yake ya huduma ili kuwarahisishia raia wa nchi za Afrika Mashariki na Kati ambao hutumia Kiswahili kama lugha ya mawasiliano.
Jovago wamefiki hatua hiyo leo jijini Dar es Salaam baada ya kuzinduwa wavuti maalum ya lugha ya Kiswahili ambayo mteja anayetafuta taarifa sahihi za hoteli kwa eneo analokwenda anaweza kuoda chumba kwa kutumia mtandao huo eneo ambalo anaelekea akiwa ugenini.
Akizungumzia mtandao huo leo katika hafla ya uzinduzi huo, Meneja wa Jovago nchini Tanzania, Andrea Guzzoni alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuona lugha ya Kiswahili inatumika katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi huku ikiwa na wadau wa sekta ya utalii wanaoitaji huduma hiyo.
Alisema hatua ya kuzinduwa tovuti hiyo ya Jovago kwa lugha ya Kiswahili ambapo mteja yoyote muitaji wa hoteli katika eneo lolote anaweza kuingia kwenye mtandao huo na kutafuta hoteli aipendayo kisha kufanya oda yake na hata malipo kwa mtandao huku akiwa huru kutumia lugha hiyo.
Alisema kwa sasa mtandao wa Jovago umefikisha matumizi ya lugha tatu kuu katika shughuli zake za kuwahudumia wateja ambapo wanatumia lugha za Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili ili kuwaunganisha zaidi wadau wa sekta ya utalii wa ndani na hata ule wa kimataifa.
“…Leo tunafurahi kufikia hatua hii ya kuingiza lugha ya Kiswahili katika huduma zetu, hili ni miongoni mwa malengo ambayo tumejiwekea yaani kuhakikisha tunawaridhisha wateja wetu kwa kutumia lugha zao ambazo ni kiungo cha mawasiliano katika maeneo yao,” alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Jovago, Paul Midy.
Akifafanua zaidi Meneja Uhusiano wa Jovago Tanzania, Lilian Kisasa alisema lengo la kampuni yao ni kuhakikisha wanachochea kukua kwa utalii wa ndani kwa kujenga mazingira rahisi ya upatikanaji wa baadhi ya taarifa wanazohitaji watalii wa ndani na hata wale wan je.
“Alisema kufunguliwa kwa huduma hiyo ya lugha ya Kiswahili pia kutachochea kiasi kikubwa kukuwa kwa sekta ya utalii hasa wa ndani ukizingatia Tanzania idadi kubwa ya wananchi hutumia Kiswahili katika shughuli zao.
Kwa sasa nchi za Tanzania, Kenya, Burundi, Rwanda na Uganda wanatumia lugha ya Kiswahili hivyo ni jambo ambalo halikwepeki matumizi yake hasa kwa maendeleo ya sekta ya utalii ambayo huwahusisha jamii nzima.
Jovago.com ni mtandao unaomuwezesha mteja kufanya oda ya hoteli aitakayo kupitia mtandao huku akipata picha halisi za hoteli aitakayo eneo na kiwango cha fedha akitakacho na anaweza kufanya malipo kupitia mtandao pia au kulipa atakapofika katika hoteli husika.
Mtandao huu una zaidi ya 25,000 nchi mbalimbali za Afrika na idadi ya hoteli 200,000 kwa duniani kote ikiwemo nchi ya Tanzania.