TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MIMI JOHN PAUL JAMBELE MGOMBEA WA NAFASI YA MWENYEKITI WA KLABU YA YANGA KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA KUJAZA NAFASI ZILIZO ACHWA WAZI NA BAADHI YA VIONGOZI WALIOJIUZULU UTAKAOFANYIKA SIKU YA JUMAPILI YA TAREHE 15/07/2012.
NIMELENGA KATIKA KUHAKIKSIHA NINASHIRIKIANA NA “WANAYANGA” WOTE NCHINI TANZANIA NA SEHEMU NYINGINE POPOTE DUNIANI KATIKA KUIFANYA KLABU HII IJITEGEMEE YENYEWE KIMAPATO NA KUPUNGUZA KWA KIASI KIKUBWA (80%) KAMA SIO KUONDOA KABISA TABIA YA KUWA TEGEMEZI WAKTI INA RASILIMALI ZA KILA AINA ZINAZOWEZA KUIFANYA IWE NA MAFANIKIO MAKUBWA SANA KATIKA KUJIENDESHA YENYEWE KIUCHUMI.
ENDAPO WANACHAMA WA YANGA WATANIPA KURA ZA USHINDI DHIDI YA WAGOMEA WENZANGU, JAMBO LA KWANZA NITAANZA NA KUTENGENEZA “MIFUMO” NDANI YA KLABU KATIKA NYANJA ZA “UTAWALA NA UONGOZI”, “NIDHAMU KATIKA MASWALA YA UTAWALA WA FEDHA”, “MIFUMO YA KUMBUKUMBU PAMOJA NA MITANDAO YA KELEKTRONIA” NA SHERIA NA KANUNIZA MANUNUZI.
KATIKA NYANJA NILIZOTAJA HAPO AWALI SHERIA, KANUNI NA MIONGOZO MBALIMBALI ITAWEKWA KATIKA MAANDISHI, HIVYO KUFANYA UTENDAJI WA SHUGHULI ZA KLABU SIKU HADI SIKU KUWA RAHISI, WENYE KUELEWEKA NA KUJENGA UWEZO KWA VIONGOZI WANAOPATA FURSA YA KUINGIA MADARAKANI WAWEZE KUIONGOZA YANGA KWA MAFANIKIO AMBAYO YANATARAJIWA NA WANAYANGA WOTE.
KATIKA KUELEKEA KWENYE KUJITEGEMEA NITAWASHIRIKISHA WANAYANGA WOTE AMBAO WANAKADIRIA KUFIKIA ZAIDI YA MILIONI KUMI NDANI YA TANZANIA NA KFUANYA SENSA YA HARAKA KUWAPATA KATI YA MILIONI HADI MILIONI TATU AMBAO WATAKUWA TAYARI KUTOA NAMBA ZAO ZA SIMU ZILIZOSAJILIWA NA KUWA TAYARI KUICHANGIA KLABU KWA KUKUBALI KUKATWA KATI YA SHILINGI 250/= HADI SHILINGI 500/= KWA WIKI ILI KLABU IWEZE KUPATA MAPATO TOKA SIMU ZAO.
HATUA INAYOFUATA NIKUTANGAZA ZABUNI KWA KAMPUNI ITAKAYOKUWA TAYARI KUSIMAMIA ZOEZI LA KUIKUSANYIA NA KUWEKA KWENYE AKAUNTI MAALUM YANGA, FEDHA TOKA KWA WANAYANGA WOTE NCHINI KOTE.
KLABU ITAHITAJI KUPATA KATI YA SHILINGI MILIONI 150 HADI 200 KWA WIKI AMBAPO IKIWA WANAYANGA MILIONI TATU WATAUMIKA BASI KLA MMOJA ATACHANGIA SHILINGI 50/= KWA WIKI NA YANGA KUPATA SHILINGI MILIONI 150/= AMBAZO KWA MWEZI ITAKUWA NI SHILINGI MILIONI 600. FEDHA NYINGINE KWENYE MAKATO HAYO ZITABAKI KWENYE KAMPUNI HUSIKA KWA AJILI YA KULIPIA KODI NA GHARAMA NYINGINE ZA UENDESHAJI.
KWA FEDHA HIZI TU AMBAZO KULINGANA NA TEKNOLOJIA YA KISASA ILIYOPO NI RAHISI SANA KUPATIKANA BILA KUJALI ENEO LA KIJIOGRAFIA ALIPO MWANAYANGA ZINAWEZA KUSAIDIA SANA KWA KLABU KUJIENDESHA YENYEWE, KULIPA MADENI YALIYOPO PAMOJA NA KUKAMILISHA MIPANGO MBALIMBALI YA MAENDELEO YA KLABU KAMA VILE UJENZI WA UWANJA WA KISASA, MAJENGO YA KISASA YA KIBIASHARA N.K.
KWA MFANO KAMA YANGA ITATUMIA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 200 KWA MWEZI KWA AJILI YA MATUMIZI YA KAWAIDA, BASI ITABAKIWA NA BAKAA YA SHILINGI MILIONI 400 KILA MWEZI KIASI AMBACHO KWA MWAKA KLABU ITAKUWA INA BAKAA YA SHILINGI BILIONI 4.8 AIDHA, KLABU ITATUMIA “LOGO” (NEMBO) YAKE KATIKA KUTANGAZA ZABUNI KWA KAMPUNI AMBAYO IKO TAYARI KUTENGENEZA/KUUZA VIFAA MBALIMBALI KWA KUTUMIA NEMBO HII KWA MFANO FULANA, BUKTA, KOFIA, SKAFU, STICKERS, TRUCKSUITS, KANGA, MIAVULI, MABEGI, KAVA ZA MATAIRI YA GARI N.K NA KUINGIA NAYO MKATABA WA MWAKA MMOJA AMBAPO VIFAA VYOTE HIVI SISI TUTAVIITA NI “SETI” MOJA.
KAMPUNI HII TUAITAKA IWE NA UWEZO WA KUTENGENEZA SETI MILIONI MOJA KWA MWAKA NA SISI YANGA TUTAHITAJI SHILINGI 3,000/= (ELFU TATU TU) KWA SETI AMBAPO KLABU ITAJIINGIZIA JUMLA YA SHILINGI BILIONI 3 KWA MWAKA. KAMPUNI ITAPEWA KIBALI CHA KUMCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA MTU YEYOTE ATAKAYEKUTWA ANAUZA VIFAA HIVI NDANI YA MWAKA HUSIKA BILA YA KIBALI TOKA KWAO. JUMLA YA BAKAA KWENYE AKAUNTI YA KLABU ITAKUWA NI SHILINGI BILIONI 7.8.
HII NI MIPANGO YA MUDA MFUPI WA KATI YA MIEZI MITATU NA SITA BAADA YA KUCHAGULIWA, NAJUA ZIPO CHANGAMOTO AMBAZO WANAYANGA WENGI ZINAWAKWAZA JUU YA UDHIBITI WA MAPATO HAYA NA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA ZOTE. NAPENDA KUWAHAKIKISHIA WANAYANGA WOTE KUWA NITAITUMIA TAALUMA YANGU KATIKA KUHAKIKISHA KUWA NIDHAMU NA UWAZI KATIKA MAPATO YA KLABU VINAKUWEPO KWA KIWANGO CHA HALI YA JUU SANA NA YAFUATAYO NITAYAFANYA:-
1. KWANZA KABISA NITAHAKIKISHA KLABU INAKUWA NA AKAUNTI NNE.
(i) AKAUNTI YA KWANZA NI AKAUNTI MAALUM (SPECIAL ACCOUNT)
AKAUNTI HII KAZI YAKE ITAKUWA NI KUPOKEA FEDHA ZOTE ZINAZOLETWA KWENYE KLABU KUPITIA VYANZO VYOTE VYA MAPATO YA KLABU.
AKUNTI HII ITAKUWA HAINA KITABU CHA HUNDI KWA KUWA NDIYO UTAKAOKUWA MFUKO MKUU WA KLABU. FEDHA TOKA KWENYE AKAUNTI HII ZITAKUWA ZIKIHAMISHWA KWA KIWANGO MAALUM AMBACHO KIMEPITISHWA NA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA BAADA YA KUWASILISHA BAJETI (MAKADIRIO) YA KLABU TOKA KWENYE KAMATI YA UTENDAJI KWENDA KWA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU.
UHAMISHAJI WA FEDHA HIZO UTAFANYIKA KWA BARUA MAALUM ILIYOAMBATANA NA MUHTASARI WA MKUTANO MKUU ULIOPTISHA MAKADIRIO HAYO. KWA HIYO AKAUNTI HII HAITAGUSWA KABISA NA MATUMIZI YA SIKU HADI SIKU YA KLABU.
(ii) AKAUNTI YA MASHINDANO
AKAUNTI HII ITAKUWA IKITUMIKA KWA AJILI YA KULIPIA SHUGHULI ZOTE ZINAZOHUSU MASHINDANO NA MICHEZO MBALIMBALI.
(iii) AKAUNTI YA USAJILI
AKAUNTI HII ITATUMIKA KWA AJILI YA KUGHARAMIA SHUGHULI ZA USAJILI WA WACHEZAJI KWA AJILI YA MWAKA UJAO NA MWAKA UNAOENDELEA WAKATI WA DIRISHA DOGO.
(iv) AKAUNTI YA UTAWALA
HII ITATUMIKA KUGHARAMIA SHUGHULI ZOTE ZA KIUTAWALA ZA KLABU KAMA VILE KULIPIA WAFANYAKAZI, VIKAO N.K.
AIDHA, TUKISHIRIKIANA NA WENZANGU NDANI YA KAMATI YA UTENDAJI NITAHAKIKISHA KWAMBA, KATIKA KUTENGENEZA MIFUMO ILI KURAHISHA UENDESHAJI WA KLABU UNAFANYIKA KWA UFANISI YAFUATAYO YATAFANYIKA:-
ZITAANDALIWA (KWA MAANDISHI) SHERIA ZA NDANI, KANUNI, TARATIBU NA MIONGOZO MBALIMBALI KUHUSU UTAWALA NA UONGOZI, UHASIBU NA UTAWALA WA FEDHA NA MANUNUZI YA BIDHAA NA HUDUMA MBALIMBALI KWA AJILI YA KLABU. MAANDIKO HAYA YATAJENGA NIDHAMU KATIKA UTENDAJI WA SHUGHULI ZA KLABU SIKU HADI SIKU NA KUWAFANYA WAHUSIKA WOTE KUWA WAADILIFU KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YA KLABU YA YANGA HASA UKIZINGATIA KWAMBA KATIKA MAANDIKO HAYA HATUA ZINAZOWEZA KUCHUKULIWA KWA WAHUSIKA KWA MAKOSA MBALIMBALI ZITAKUWA ZIMEAINISHWA PAMOJA NA JINSI ZITAKAVYOWEZA KUTEKELEZWA.
PIA NIKIPATA NAFASI HII NINAYOIGOMBEA, NITAHAKIKISHA KUWA NINAANDAA TAARIFA YA FEDHA (FINANCIAL STATEMENT) KILA MWAKA WA FEDHA UNAPOKAMILIKA NA KUIWASILISHA KWENYE MKUTANO MKUU WA WANACHAMA BAADA YA KUKAGULIWA NA MKAGUZI WA NJE (EXTERNAL AUDITOR) ATAKAYEKUWA AMETEULIWA NA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA WA KLABU YA YANGA. NITAHAKIKISHA NATOA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YA KILA MIEZI MITATU NA KUZISAMBAZA KATIKA MATAWI PAMOJA NA TAARIFA YA UTEKELEZAJI (PERFORMANCE REPORT) ILI WANAYANGA WAELEWE KINACHOENDELEA NDANI YA YANGA NA KUIFANYA KLABU IENDESHWE KWA UWAZI NA UADILIFU WA HALI YA JUU KABISA.
KATIKA UTAWALA NITAHAKIKISHA KUWA MATAWI NINAYAPA NGUVU YA HALI YA JUU KATIKA KUSHIRIKI KUCHEZA MECHI ZA LIGI NA MASHINDANO YA KIMATAIFA KULINGANA NA MAKUBALIANO TUTAKAYOYAFANYA NA VIONGOZI WA MATAWI. NITAJITAHIDI KUYAWEZESHA KWA NGUVU ZOTE. HII NINA MAANA HATA MATAWI YALIYOPO MIKOANI NITAYAPA NAFASI HASA KWA MICHEZO INAYOCHEZWA KATIKA MIKOA YAO.
NAPENDA KUAHIDI PIA KUWA, ENDAPO NITAPEWA NAFASI YA KUWA MWENYEKITI WA KLABU YA YANGA NITAHAKIKISHA NINAVUNJA MAKUNDI NDANI YA KLABU NA KUIFANYA IWE NA UMOJA WA HALI YA JUU KWA KUMPA KILA MWANACHAMA NAFASI YA KUSIKILIZWA NA KUSHAURIANA NAYE KWA UWAZI NA UPENDO. KATIKA KIPINDI CHA UTAWALA WANGU KAMA NITACHAGULIWA NITAHAKIKISHA KLABU INAKUWA NA TIMU BORA SANA YA VIJANA AMBAO WATAKUWA WAKILELEWA TANGU WAKIWA NA MIAKA 15 HADI WAFIKAPO MIAKA 21 AMBAPO WATAPEWA KILA AINA YA USHIRIKIANO NA MATUNZO ILI IWE NI CHANZO KIZURI CHA TIMU YA KLABU YA YANGA KWA VIPINDI TOFAUTI VYA USAJILI.
AIDHA, NITAHAKIKISHA KWA KUSHIRIKIANA NA KAMATI YA UTENDAJI, VIONGOZI WA MATAWI, WANACHAMA PAMOJA NA WANAYANGA WOTE, TIMU YETU INAKUWA IKICHUKUWA UBINGWA WA TANZANIA KILA MWAKA, AFRIKA MASHARIKI NA KATI PAMOJA NA KUSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA KWA MAFANIKIO YA HALI JUU SANA. KUHUSU UANZISHWAJI WA KAMPUNI NITAHAKIKISHA KLABU YA YANGA INAANZISHA KAMPUNI AMBAYO INADHAMINIWA NA HISA ZA WANACHAMA NA SI DHAMANA ZA KLABU ILI HATA KAMA IKITOKEA KWA BAHATI MBAYA KAMPUNI KUFILISIKA BASI RASILIMALI ZILIOTOKANA NA HISA TU NDIYO ZITAKAZOFILISIWA, LAKINI MALI ZA KLABU ZITABAKI SALAMA SALIMINI. MCHAKATO HUU NITAUSIMAMIA KWA KASI ILI KLABU IWEZE KUJIONGEZEA MAPATO ZAIDI.
KATIKA MAKUBALIANO NITAPENDEKEZA KWAMBA NUSU YA FAIDA ITAKAYOPATIKANA BAADA YA KUTOA KODI, ITALETWA KWENYE AKAUNTI MAALUM YA KLABU NA NUSU ILIYOSALIA ITABAKI KWENYE KAMPUNI KWA AJILI YA MAAMUZI YA WANAHISA. AIDHA, NITAHAKIKISHA KUWA MIKUTANO YOTE YA KIKATIBA INAFANYIKA NA KWA MUJIBU WA TARATIBU NA NDANI YA KANUNI ZA UTAWALA NA UONGOZI UTAWEKA UTARATIBU WA KUITISHA MIKUTANO YA WANACHAMA ILI KUUBANA UONGOZI UWEZE KUTEKELEZA MATAKWA YA KIKANUNI KWA KUONYESHA NI WIKI YA NGAPI YA MWEZI GANI MIKUTANO INAPASWA KUWA IMEFANYIKA. PIA, KATIKA MIKUTANO HII YA WANACHAMA TUTAJITAHIDI KUHAKIKISHA KUWA BAADHI YA VIPENGELE VYENYE KASORO KATIKA KATIBA YA SASA VINAFANYIWA MABORESHO.
MWISHO NAPENDA KUOMBA KURA KWA WANACHAMA WOTE WA YANGA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 15/07/2012 ILI NIWE MWENYEKITI WENU KWA AJILI YA KUIJENGA YANGA ILIYO IMARA KIUCHUMI NA KIMCHEZO.
NAWASHUKURU WOTE.
JOHN P. JAMBELE
MGOMBEA – UENYEKITI KLABU YA YANGA
TAREHE 12/07/2012