JK Kuwaleta Wafanyabiashara wa Oman Tanzania

The Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Bernard Membe and Oman Ministry of Financial Affairs Secretary General, Sultan bin Salim Al Habsi sign and exchange legal instruments.

Na Mwandishi Maalumu, Oman

SERIKALI ya kifalme ya Oman inatarajia kutuma ujumbe wake ambao utajumuisha na wafanyabiashara kuja Tanzania kutathmini na kuangalia maeneo gani nchi hiyo na wafanyabiashara wake wanaweza kuwekeza, kufuatia ziara ya kiserikali ya Rais Jakaya Kikwete ya siku 4 nchini Oman.
“Tutaunda kamati na kutuma ujumbe kwenda Tanzania kuangalia na kujua aina gani ya biashara na vitega uchumi Oman inaweza kuwekeza”. Amesema Naibu Waziri Mkuu wa Serikali ya kifalme ya Oman, Sayyid Fahad Mahmood Al Said wakati wa mazungumzo yao ya Kiserikali.

Naibu Waziri Mkuu huyo amesema Oman ina matumaini makubwa kuhusu mazungumzo yao ya Octoba 17, 2012 yaliyofanyika katika makao makuu ya Baraza la Mawaziri. Amesema Baraza la Mawaziri la nchi yake litakaa na kujadiliana pamoja na Chama cha wafanyibiashara na Viwanda kuandaa Serikali ya kuja Tanzania na kuhakimisha mahusiano yetu yanadumu.

Rais amemueleza Makamu wa Waziri Mkuu kuwa Tanzania hivi karibuni imegundua gesi kwa wingi na hivyo kuna changamoto kubwa ya kujenga uwezo kwa watu wake waweze kujadiliana na kuwekeana mikataba itakayoleta tija kwa Taifa na watu wake. Rais Kikwete pia amekutana na watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchini Oman ambapo amewaeleza kwa kifupi maendeleo yanayoletwa na Serikali katika Nyanja za Kilimo, Elimu, Afya, miundombinu na mambo mbalimbali ya kisiasa yanayoendelea nchini Tanzania.

Watanzania hao, nao wamepata nafasi ya kuelezea matatizo na matarajio yao kwa Rais, ambapo Rais amewapata nafasi ya kufafanua na kujibu baadhi ya hoja zao na kuwapa changamoto watanzania wote wanaoishi nchi za nje ya kushiriki katika shughuli za maendeleo na kukuza Uchumi wa Tanzania kwa kutafuta na kushawishi wawekezaji na marafiki mbalimbali kusaidia katika nyanja mbalimbali ambazo zinahitaji misaada ya maendeleo. Rais anamaliza ziara yake tarehe 18 Octoba, 2012 na kurejea nyumbani jioni.