JK Katika Msiba wa Nelson Mandela Afrika Kusini

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Rais Barack Obama wa Marekani kwa viongozi mbalimbali wa Afrika wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya Mzee Nelson Mandela Uwanja wa FNB jijini Johannesburg Jumanne Novemba 10, 2013. PICHA NA IKULU.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya Mzee Nelson Mandela Uwanja wa FNB jijini Johannesburg Jumanne Novemba 10, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya Kumbukumbu ya Mzee Nelson Mandela Uwanja wa FNB jijini Johannesburg Jumanne Novemba 10, 2013

NGI_3523
DSC04695

Taswira za siku Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete walipomtembelea Mzee Nelson Mandela jijini Pretoria enzi za uhai wake. PICHA NA IKULU

Taswira za siku Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete walipomtembelea Mzee Nelson Mandela jijini Pretoria enzi za uhai wake. PICHA NA IKULU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Desemba 10, 2013, aliungana na viongozi wa mataifa mbali mbali duniani na maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Nelson R Mandela.

Maelfu kwa maelfu ya wananchi wamehimili mvua kubwa iliyokuwa inanyesha kwa nguvu kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg kumwaga Mzee Mandela ambaye alikuwa ishara kuu ya upinzani wa siasa za ubaguzi wa rangi za makaburu wa Afrika Kusini. Mandela ambaye alifariki duniani Ijumaa iliyopita, Desemba 5, 2013, alikuwa Kamanda wa Jeshi la Ukombozi la Chama cha African National Congress la Umkhoto we Sizwe akafungwa jela kwa uhaini kwa miaka 27 na utawala wa Makaburu.

Baada ya kutoka jela Februari 1990, Mzee Mandela alichaguliwa kuwa Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini ya mwaka 1994. Lakini Mandela alitumikia kipindi kimoja tu cha miaka mitano na kukataa kutumikia kipindi cha pili. Kiasi cha viongozi 91 kutoka sehemu duniani wamehudhuria Kumbukumbu hiyo iliyokuwa na kila aina ya mchanganyiko wa hisia – wengine wakiwa na majonzi na wengine wakicheza na kuimba kwa muda wote wa shughuli hiyo iliyochukua kiasi cha jumla ya saa tano.

Mbali na Rais Kikwete ambaye amefuatana na Mama Salma Kikwete, marais wengine mashuhuri duniani waliohudhuria Kumbukumbu hiyo ni Barack Obama wa Marekani, Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroun na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon. Kumbukumbu hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa zamani wa Marekani wakiwemo marais watatu wa zamani wa Marekani – Jimmy Carter, Bill Clinton na George W. Bush na mawaziri wakuu wawili wa zamani wa Uingereza, Tony Blair na Gordon Brown.

Rais Kikwete, siku iliyofuata aliungana na viongozi wenzake katika kutoa heshima za mwisho na kuuaga rasmi mwili wa Marehemu Mandela ambao utawekwa kwenye Majengo ya Urais wa Afrika Kusini ya Union Buildings mjini Pretoria.