JK, Dk Bilal Aongoza Waombolezaji Kumuaga Dk Shija

Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Marehemu Dk. William Shija alipoongoza shughuli za kuaga Oktoba 12, 2014 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dk. William Shija, wakati wa zoezi la kuagwa mwili lililofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Oktoba 12, 2014. Picha na OMR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mrisho Jakaya Kikwete, akiwafariji wanafamilia wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dk. William Shija, wakati wa zoezi la kuagwa mwili lililofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Oktoba 12, 2014. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mrisho Jakaya Kikwete, akiwafariji wanafamilia wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dk. William Shija, wakati wa zoezi la kuagwa mwili lililofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Oktoba 12, 2014. Picha na OMR

Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu. 

Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu. 

Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Makamu wake Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati wakiwa katika Viwanja vya Karimjee wakijumuika na waombolezaji wengine katika zoezi la kuagwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dk. William Shija, Oktoba 12, 2014. Picha na OMR

Askari wa Bunge la Jamhuri, wakibeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dk. William Shija, wakati wakiwasili kwenye viwanja vya Karimjee kwa ajili ya zoezi la kuagwa mwili, Oktoba 12, 2014. Picha na OMR

Rais Kikwete Amwaga Marehemu Dk. Shija
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete Oktoba 12, 2014, ameungana na waombolezaji kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa Katibu Mkuu wa Kwanza Mwafrika wa Chama cha Mabunge ya Jumuia ya Madola (CPA) Dk. William Ferdinand Shija, ambaye pia alipata kuwa Waziri Mwandamizi wa Serikali, katika shughuli iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Rais Kikwete amewasili kwenye Viwanja vya Karimjee kiasi cha saa 4:10 asubuhi kujiunga na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Mwenyekiti wa CPA-Kanda ya Afrika Anne Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania, viongozi na wananchi kutoa heshima za mwisho.
Baada ya kuaga mwili, Rais Kikwete ametia saini Kitabu cha Maombolezo ya Dk. Shija ambaye alifariki dunia Jumamosi ya wiki iliyopita, Oktoba 4, 2014 kwenye Hospitali ya Charing Cross mjini London, Uingereza ambako alikuwa anapata matibabu ya ugonjwa wa Saratani. Makazi yake ya kazi yalikuwa huko huko Uingereza.
Miongoni mwa waombolezaji wengi kwenye shughuli hiyo ya leo ulikuwa ni ujumbe mzito wa CPA ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Lindiwe Maseko wa Afrika Kusini. Pia shughuli hiyo imehudhuriwa na Bwana Joe Omoldin ambaye sasa ni Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hicho.
Dk. Shija ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Nyalukomba, Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza, Aprili 28, Mwaka 1947, alipata elimu ya awali maeneo ya kwako kabla ya kujiunga na Sekondari ya Chopra mjini Mwanza kwa elimu ya sekondari na kuhitimu ualimu katika Chuo cha Ualimu cha Chan’gombe cha Dar es Salaam Mwaka 1968.
Baadaye, Dk. Shija alipata Shahada ya kwanza ya Uzamili ya Uandishi wa Habari nchini India kabla ya kupata Shahada ya Uzamivu ya fani hiyo hiyo ya Uandishi wa Habari katika Chuo Kikuu cha Howard cha mjini Washington, D.C., Marekani. Wakati wote wa masomo yake alikuwa Mhadhiri wa Uandishi kwenye Chuo cha Nyegezi, Mwanza.
Dk. Shija aligombea na kushinda Ubunge wa Jimbo la Sengerema Mwaka 1990 na kuingia Serikali ambako alishikilia nafasi tofauti kwa vipindi tofauti kama Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Waziri wa Habari na Utangazaji, Waziri wa Nishati na Madini na Waziri wa Biashara na Viwanda. Dkt. Shija pia amepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Katika Mkutano Mkuu wake wa 52, Desemba, Mwaka 2006 mjini Abuja, Nigeria, Dk. Shija alichaguliwa, baada ya mchuano mkali sana, kuwa Katibu Mkuu wa Kwanza Mwafrika wa CPA, taasisi ambayo tokea kuanzishwa kwake Mwaka 1911 ilikuwa haijapata kumchagua Mwafrika kuwa Mtendaji Mkuu wake.
Alichaguliwa kwa kipindi cha pili Mwaka 2012 baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano. Alikuwa anamaliza muda wake Desemba 2016.
Mpaka anaaga dunia, Dk. Shija alikuwa ameshikilia nafasi ya Ukatibu Mkuu wa CPA kwa mafanikio makubwa sana kwa miezi saba na miezi tisa. Atazikwa kesho, Jumatatu, Oktoba 13, 2014 katika kijiji cha kwao cha Nyalukomba, Sengerema, Mwanza.