JK awasili Kilimanjaro kwa ziara ya siku 3

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa kwa furaha mara alipotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jioni hii. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama. Picha na Ikulu.

Na Mwandishi Maalumu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Moshi Machi 4, 2012 tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo.

Miongoni mwa shughuli ambazo Rais atafanya ni pamoja na kuzindua kampeni ya kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo ataizindua kwa kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro Speak Out, Climb Up”.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea taaria ya Mkoa toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama mara tu baada ya kuwasili Ikulu ndogo mjini Moshi jioni hii. PICHA NA IKULU


Shughuli hiyo itakayofanyika Machi 5, 2012 asubuhi, imepangwa kwenye Lango la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA). Mbali na kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua Mkutano wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi mjini Moshi.

Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea Mkoa huo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.