
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mtoto Maganga mwenye umri wa miaka mitatu ambaye pamoja na mama yake walikuwa katika mojawapo ya vikundi kadhaa vya ngoma za asili zilizomlaki uwanja wa ndege wa Mwanza leo January 4, 2012 alikotua tayari kwa kujiunga na wana CCM kusherehekea miaka 35 ya chama hicho tawala.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa katika uwanja wa ndege wa Mwanza leo January 4, 2012 alikotua tayari kwa kujiunga na wana CCM kusherehekea miaka 35 ya chama hicho tawala. (Picha na Ikulu)

Rais Jakaya Kikwete akishuka kwenye ndege alipowasili Uwanja wa Ndege wa Mwanza leo jioni. (Picha na Bashir Nkoromo)

Katibu wa NEC Itikadoi na Uenezi Nape Nnauye akimbusu mtoto Nyambani Mganga (3) baada ya kuviwa na uchezaji ngoma wake, katika kikundi cha Utandawazi Theatre cha Ukerewe, kilipokuwa kikitumbuza kabla kabla ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza leo kwa ajili ya maadhimhso ya miaka 35 ya CCM kesho.