Rais Jakaya Kikwete akiangalia aina za mafuta katika banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, TPDC (kulia) na kushoto anayeeleza ni Mgeolojia Ibrahim Rutta, wakati akitembelea maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha zote na Magreth Kinabo – Maelezo.
Rais Jakaya Kikwete akitoka katika Banda la Tanzania na kuingia banda la Benki Kuu ya Tanzania (BOT) huku akisaliana na baadhi ya viongozi wa BOT, wakati akitembelea maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha zote na Magreth Kinabo – Maelezo.
Rais Jakaya Kikwete akisisitiza juu ya utoaji wa elimi wa kilimo cha kisasa kwa wananchi baada ya kuona bustani bora ya kilimo cha nyanya katika banda la Jeshi la Magereza (kulia) kwa Sajenti Nicolas Sikazwe wa jeshi hilo kushoto wa jeshi hilo, wakati akitembelea maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J. K. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiangalia shamba la mahindi katika banda la Jeshi la Magereza (kushoto) na kulia ni Kamishna Gaston Sanga wa jeshi hilo, wakati akitembelea maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akiangalia (katikati)sahani ambazo si rahisi kuvunjika(kushoto) ni Sohaic Ahamed kutoka Pakstan, kwenye banda la Karume wakati akitembelea maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha zote na Magreth Kinabo – Maelezo.
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
RAIS Jakaya Kikwete amewataka wafanyabiashara nchini kuongeza juhudi za kuboresha ubora wa bidhaa zao ili ziweze kushindana na zile za nje ya nchi. Rais Kikwete amewapongeza washiriki wa maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa kwa kuongeza ubora wa bidhaa ambao kila mwaka kumekuwa na tofauti.
Kauli hiyo imetolewa na Rais Kikwete wakati akitembelea maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Maonesho ya mwaka huu yamepiga hatua kubwa kwani kumekuwepo kwa ongezeko la bidhaa, bidhaa zimefungwa vizuri tukiendelea hivi tunaweza kushindana na bidhaa za kimataifa. Pendekezo langu mimi ni kuendelea kufanya ziwe vizuri zaidi,” alisema Rais Kikwete.
Akitembelea banda la Jeshi la Magereza, Rais Kikwete ambapo alijionea uzalishaji wa bidhaa za kilimo, alilitaka jeshi hilo kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo bora cha kisasa. Katika ziara hiyo Rais Kikwete alitembelea mabanda mbalimbali likiwemo la Wakala wa Mafunzo nje ya nchi. Benki Kuu ya Tanzania, Bidhaa za Tanzaniana mengineyo.