JK Apokea Ujumbe Maalumu wa Rais Jacob Zuma

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono  na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam. Picha na IKULU.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono  na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam. Picha na IKULU.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, Machi 16, 2014, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

Ujumbe huo wa Rais Zuma umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane wakati mama huyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.

Mara baada ya kuwasilisha ujumbe huo, viongozi hao wamejadili masuala yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini na masuala ya kikanda ambako nchi zote mbili ni wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mheshimiwa Nkoana-Mashabane amendoka nchini mara baada ya kuwa amewasilisha ujumbe huo kwa Rais Kikwete.