
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi hayo kutoka kwenye Ofisi ya CCM Mkoa wa Mwanza hadi viwanja vya Furahisha jijini Mwanza akiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa CCM. Kutoka Ofisi hiyo hadi kwenye viwanja hivyo ni umbali wa kilometa tatu.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza kuongoza matembezi ya mshikamano kwa ajili ya maadhimnisho ya miaka 35 ya CCM leo asubuhi. Anayempokea ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na wengine ni Spika wa Bunge Anna Makinda ambaye ni mlezi wa mkoa huo na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama. Pamoja na Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Clement Mabina na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilllo.