RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Zahor Kassim Mohamed EL-KHAROUSY kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi katika Bahari Kuu. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kutiwa saini, Desemba 7, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa uteuzi wa Bwana El Kharousy ulianza Novemba 28, mwaka huu, 2012. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kharousy alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo.