JK Amteuwa Jaji Amiri Msumi Kuwa Bosi Baraza la Maadili

Rais Jakaya Kikwete



RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji na Balozi Mstaafu Mheshimiwa Hamis Amiri Msumi kuwa Mwenyekiti wa BARAZA LA MAADILI.
Taarifa iliyotolewa 26 Februari, 2013 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Februari 18, mwaka huu, 2013.