Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 5(51) cha Sheria ya Majukumu ya Mawaziri The Ministers (Discharge of Ministerial Functions)Act, sura ya 299 ameanzisha Chombo cha Kusimamia Ufuatiliaji wa utekelezaji wa program na Miradi ya Maendeleo kwenye Maendeo ya Kimkakati ya Kitaifa (National Key Result Areas) kinachojulikana kama “President’s Delivery Bureau (PDB)”.
PDB itakuwa chini ya Ofisi ya Rais, Ikulu na itakuwa na majukumu yafuatayo:-
• Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Programu na miradi kwenye Maeneo ya kimkakati ya Kitaifa yanayohitaji matokeo ya haraka.
• Kuwezesha ufafanuzi wa kina na program kwenye maeneo ya Kimkakati ya Kitaifa yanayohitaji matokeo ya haraka.
• Kuwezesha na kufanikisha kuanzisha program na miradi kwenye Maeneo ya Kimkakati ya Kitaifa yanayohitaji matokeo ya haraka.
• Kuwezesha kutambua na kuainisha Maeneo ya Kimkakati ya Kitaifa yanayohitaji matokeo ya haraka.
• Kusaidia kutoa uchambuzi na mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto maalum za utekelezaji.
• Kushirikisha umma kwenye Program na miradi iliyoainishwa kwenye maeneo ya kipaumbele.
• Kuandaa taarifa za utendaji kwa kipindi maalum kwenye Maeneo ya Kimkakati ya Kitaifa na kuziwasilisha kwenye mamlaka husika.
• Kutoa ushauri wa kitaalam wa ndani na kuishauri Serikali kwenye maeneo ya Kimkakati ya Kitaifa.
• Kupanga na kusimamia uendeshaji wa shughuli za ‘Labs’.
• Kuwezesha usimamizi wa mikataba ya utendaji kwa Mawaziri wanaouhusika na program na miradi ya kipaumbele iliyo chini ya Wizara zao.
• Kuwezesha na kusimamia uandaaji wa viashiria vikuu vya utendaji (Key Performance Indicators) vya kitaifa na kiwizara kwenye program na miradi ya kipaumbele.
• Kufanya uhakiki wa utendaji wa Mawaziri kwenye Maeneo ya Kimkakati ya kitaifa yanayohitaji matokeo ya haraka.
• Kuwezesha uhakiki wa utendaji wa PDB.
Aidha, taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kwamba, Mheshimiwa Rais pia amemteua Ndugu OMARI ISSA kuwa Mtendaji Mkuu wa kwanza wa PDB kuanzia tarehe 01 Juni, 2013.
Ndugu Omari Issa ni Mtanzania mwenye uzoefu mkubwa ndani na nje ya nchi, barani Afrika na duniani, kwenye sekta ya umma na sekta binafsi, na kwenye ulimwengu wa biashahra na utendaji wa makampuni makubwa ya kimataifa. Mheshimiwa Rais anaamini kuwa uzoefu huo na utamaduni huo wa utendaji katika sekta binafsi katika ngazi hiyo utakuwa mchango mkubwa na muhimu katika siku za mwanzo za President’s Delivery Bureau na ubadilishaji wa utamaduni wa utendaji Serikalini kwenye maeneo ya kipaumbele. Ndugu OMARI ISSA alikuwa Mtendaji Mkuu wa kwanza wa “Investment Climate Facility for Africa”.
Wasifu wake