JK akiwasili nchini Uganda


Rais Jakaya Kikwete amewasili nchini Uganda kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni zinazofanyika Uganda leo. Museveni anaapishwa baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Februari mwaka huu na kumshinda mpinzani wake mkuu Kizza Besigye.

Pichani juu ni Rais Jakaya Kikwete akipokelewa kwa maua muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe Uganda tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni. Marais wengine waliowasili Kampala jana ni pamoja na Goodluck Jonathan wa Nigeria na, Robert Mugabe wa Zimbabwe na viongozi wengine na wawakilishi wa marais walitarajiwa kuwasili baadaye kuhudhuria sherehe hizo. (Picha na Freddy Maro)