JK Akihani Msiba wa Mabomu Arusha

Wananchi wakimuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete baada ya kumtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7,

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa marehemu Regina Longino Kurusei (45), mkazi wa Olasiti aliyefariiki katika shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu alipowasili katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti Jumapili iliyopita