JK Aipa Pole Familia ya Mwalimu Nyerere kwa Msiba

Mama Maria Nyerere

Mama Maria Nyerere


RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salama za rambirambi kwa mama Maria Nyerere na familia yake kwa kuondokewa na mmoja wa wana familia yake, Bw. John Nyerere aliyefariki Mei 9,2015 katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam Pamoja na salamu hizi, Rais Kikwete ambaye yuko nchini Alrgeria kwa ziara ya kikazi, amefanya mawasiliano binafsi na Mama Maria na kumpa pole kwa kuondokewa na kijana wake.

“Hakuna mzazi anayependa kuondokewa na mwanae, ni kitu kigumu sana kwa mzazi kukishuhudia , hivyo naelewa maumivu na huzuni kubwa uliyo nayo”. Rais amemwambia Mama Maria na kumuomba akaze moyo na kumuombea Marehemu John apate pumziko la milele.

Rais Kikwete amemhakikishia Mama Maria kuwa yeye binafsi pamoja na familia yake , wapo nae katika kipindi hiki kigumu na kuwa watashirikiana wote katika msiba huu kwa hali na mali.